Wednesday, July 1, 2009

MWILI WA MICHAEL JACKSON KURUDISHWA NEVERLAND LEO

Mwili wa Michael Jackson leo utarudisha kwenye ranchi yake ya Neverland California ambapo utawekwa na kutoa nafasi kwa umma kutoa heshima za mwisho mwishoni mwa wiki, vyombo vya habari vimeripoti. Utawekwa hadharani ukiwa katika katika jeneza la kioo, na kuzikwa kwenye shamba lake mwishoni mwa wiki.

Mwili wake ukiwa kwenye jeneza utawekwa kwenye kagari Keupe cha kukokotwa kwa farasi mweupe ambaye amefundishwa kukokotwa kigari hicho.

Umati mkubwa wa watu unatarajiwa kushuhudia jeneza la Mfalme wa Muziki wa Pop wakati likipita katika mitaa ya jiji la Los Angeles, kuanzia saa nne asubuhi.

Kisha kutakuwa na msafara wa magari 30 kuelekea nje ya mjini katika ranchi ya Neverland ambayo ipo karibu na mji wa Los Olivos kaskazini mwa Santa Barbara.


Watu wa usalama wa California Highway Patrol wamepanga ulinzi mkali katika msafara huo unaoanzia Los Angeles nyumbani kwa familia ya Jackson mpaka Neverland Valley.

No comments:

Post a Comment