Wednesday, July 1, 2009

kUNDI JIPYA LA TAARABU LAANZISHWA DAR, LIMEWAKOMBA WASANII MUHIMU KUTOKA JAHAZI, MELODY NA ZANZIBAR STARS.

Kikundi kipya cha taarabu Tanzania 'Five star morden Taarab' kimeanzishwa jijini Dar es salaam, kwa mujibu wa bwana Slim ambae pia ni mmiliki wa ukumbi wa Equator Grill uliopo Mtoni sabasaba kundi hilo tayari limeanza mazoezi ya nyimbo zao.

Five star imeundwa na wasanii mahiri wa muziki huo wa mitikisiko ya pwani ambao wametokea kwenye vikundi vya Jahaz, New Zanzibar stars, na East African melody kiasi cha kutia hofu kwa vikundi hivyo kupokonywa washabiki na umaarufu wao hususan wa Jahazi.

Muziki wa taarabu una wapenzi wengi sana siku hizi hasa sehemu za mwambao kiasi cha kuvutia hata wasanii wa muziki wa kizazi kipya kufanya aina hiyo ya mziki, mfano mzuri ni msanii HAMMER Q, na Q CHIEF.

No comments:

Post a Comment