Friday, July 3, 2009

MREMBO VYUO VIKUU TZ KUPATIKANA LEO, KARIMJEE DSM

Mashindano ya 'Miss higher learning 2009' yanatarajiwa kufanyika leo ijumaa tarehe 3 july katika ukumbi wa Karimjee Da es Salaam yatashirikisha warembo 12 watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo.

Mratibu wa Mashindano hayo Manka Mushi pichani ambae alishiriki Miss Tz 2003 alisema mshindi atapewa sofa lenye thamani ya sh. milioni 1.5 na pesa taslim sh.500,000.
Alisema mshindi wa2 atapewa fanicha zenye thamani ya sh. milioni moja na pesa taslim 350,000, mshindi wa3 sh. 250,000 na fanicha zenye thamani ya sh.500,000, mshindi wa4 sh.200,000 na manunuzi ya mavazi kutoka Zizzou Fashion yenye thamani ya sh 150,000 na mshindi wa5 atapewa sh.100,000 na zawadi kutoka duka la nguo la City Stars huku washiriki waliobaki wakipata kifuta jasho cha sh.50,000 kila mmoja.

Mashindano hayo yatasindikizwa na burudani kutoka bendi ya muziki wa dansi ya Afrika Stars ya Twanga Pepeta ambapo kwa mujibu wa mnenguaji Luiza Mbutu alisema bendi hiyo itapiga vibao vyake vipya vilivyozindulkiwa katika uzunduzi wa Albamu ya 'Mwana Dar es Salaam'.

Washiriki watakaowania taji hilo ni pamoja na Mwantumu Yusuph, Beatrice Kinyto, Linda Mzinga, Magreth Beatus, Doris Deonatus, Jenny Rapoo, Easther Gao, Frabcisca Mansilo, Beatrice Lukindo, Aisha Ricoh na Veronica Mick.

Wadhamini wa mashindano hayo ni Vodacom, Sabmiler, Ben Expendition Tour, Air Tanzania, Ndege Insurance, Tsco Fanicha, Perfect Solution, Rozela Saloon, City Star Botique, Dollywood, Girafe Ocion View, Aurora Segurity, Carpuany Design pamoja na Fullshangwe BlogSpot ya bwana John Bukuku.

No comments:

Post a Comment