Friday, July 3, 2009

KUNDI LA HIPHOP YA KIISLAM "NATIVE DEEN" KUPERFORM BONGO

Lile kundi la Muslim hiphop kutoka Washington Marekani 'Native Deen' linatarajiwa kuzuru ndani ya bongo tarehe 6 mwezi huu umeripoti ubalozi wa Marekani jijini DSM, jamaa wanakuja kwa minajili ya kufanya show 3 za hiphop ya style yao, huku show 2 zikilenga ktk kujikinga na maambukizi ya virusi HIV/AIDS dhidi ya vijana.
Native deen wakiwa kwenye show Palestina
Ratiba ya maonyesho yao ni km ifuatavyo:-
July 8th at 11:00pm, Zanzibar International Film Festival (ZIFF), Zanzibar;
July 10th at 1:30pm, Maisara Grounds, Zanzibar;
na July 11th at 4:00pm, Leader’s Club, Dar-es-Salaam.

Matamasha yote yatakua ya wazi na bure kwa kila mtu.

kwenye onyesho Uturuki

Kundi hilo lenye wasanii wa3 JOSHUA, NAEEM na A.MALIK limeshawahi kufika hapa nchini na kufanya show km hizi tarehe za 11 na 12 July 2007.

No comments:

Post a Comment