Friday, July 3, 2009

AY, PROF. JIIZE, NA SHAA KUPAMBANISHWA AGOSTI 7, MSHINDI KUSHIRIKI TUZO ZA MUZIKI ZA ZAIN & MTV AFRICA 2009


Kampuni ya Zain na MTV Network Africa watafanya tamasha la muziki Tanzania wakiwa ktk maandalizi ya Tuzo za muziki za MTV Afrika na Zain 2009 kwa mara ya pili ambazo zitafanyika Nairobi nchini Kenya Oktoba 10 mwaka huu.


Tamasha hilo la kipekee litakalo ambatana na shoo za madj wa klabu mbalimbali, litasaidia kwa namna 1 au nyingine ktk kuendeleza muziki wa Tanzania pia litafanyika shindano la kumsaka msanii bora kati ya Profesa Jay, AY na Shaa atakayepatikana mshindi atapelekwa nchini Kenya kushuhudia tuzo za muziki za MTV Afrika na Zain zitakazo fanyika Oktoba 10 mwaka huu.


Mshindi kati ya hao wasanii atapatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki wa muziki Tanzania kutumia ujumbe mfupi wa maneno kutika simu zao za mkononi kuanzia Julai 29 na Agosti 7, ataiwakilisha nchi kwenye tuzo za MAMA 2009.

No comments:

Post a Comment