Tuesday, June 30, 2009

KIKUNDI CHA WATOTO YATIMA KUWAKILISHA ZANZIBAR KWENYE " MALTA GUINESS STREET DANCE AFRICA COMPETITION 2009 "

Kikundi cha Watoto wa mitaani cha B6 kimeibuka bingwa wa kucheza dansi kwa visiwa vya Zanzibar na kukabidhiwa fedha taslimu sh. 600,000 katika mashindano ya Street dance yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe, visiwani humo.

Kikundi hicho ndicho kitakachoiwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya Taifa yatakayofanyika mapema Agosti, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diomond Jubilee, Dsm.
Meneja wa kinywaji cha Malta Gueness, Sara Munena alisema mashindano hayo yalivuta hisia za watazamaji kutokana na vipaji vilivyooneshwa na vikundi vilivyoshiriki ambapo karibu kila kikundi kilikuwa na uwezo sawa na kikundi kingine. Washindi wa2 walipewa shs.200,000 na wa3 shs. 100,000.

Baada ya kupata washindi katika visiwa hivyo, Julai 4 mwaka huu watafanya mashindano katika jijini Arusha, Julai 19 jijini Dar es Salaam ambapo baada ya kumalizia katika mikoa hiyo, fainali zake zitafanyika Agosti Mosi, Diomond Jubilee, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment