Baadhi ya wasaanii na wadau mbalimbali wakionyesha msimamo ktk kusimama pamoja ili kuwachangia wenzetu wakazi wa mbagala walioathilika na mabomu yaliyo na yanayoendelea kulipuka, walipokuwa ktk mkutano wa pamoja na waandishi wa habari jana.
Sambamba na show kali kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki zaidi ya 60, pia kutakuwa na mechi kali ya hisani kati ya Simba SC na Lyon Sport ya Mbagala ktk uwanja huohuo wa taifa zamani a.k.a shamba la bibi.
Kiingilio kitakuwa Shs. 3000 kawaida na Shs. 5000 viti maalum kwa wakubwa, watoto watachangia Shs. 1000 tu. Pia Kuna tiketi maalum kwa ajili ya kuchangia kwa hiari Shs.50,000 .
Muda ni kuanzia saa 3 asubuhi mpaka 12:30 jioni.
Wasanii watakao kuwepo kwenye tamasha hilo ni pamoja na AY, PROF JAY, NAKAAYA, DKNOB, WANAUME HALISI, WANAUME TMK, MKOLONI, GSOLO, TMK UNITY, MAJITA, DULLAYO, MZEE YUSUPH, OMARY TEGO, DOGO MFAUME, OMARY OMARY, OMMY G, KIKOSI CHA MIZINGA, ZOLA D, NGWAIR, FM ACADEMIA ,AKUDO, BUSHOKE, DULLY, MB DOG , LWP, KALA JEREMIAH, MACHOZI, MAUNDA ZORRO, PIG BLACK, DAN MSIMAMO NA WENGINE KIBAO.
TWENDE MDAU TWENDE TUKACHANGIE TWENDE TUSIMAME PAMOJA!!!
No comments:
Post a Comment