Wanamuziki Banana Zorro, Frola Mbasha na Paoul Ndunguru walipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar.
Jumapili ya kesho kutwa 7 june pale Coco beach kutakua na tamasha la bure kabisa la uzinduzi wa albamu ya mseto ya wahapahapa kutoka kwa wasanii kibao wenye majina makubwa na waliofanya kazi kubwa kwenye huu ulimwengu wa sanaa ya muziki wa kitanzania.
Wasanii hao mchanganyiko wamefanya nyimbo zinazopingana na ukimwi na kufanya albamu ya pamoja ya Wahapahapa. Wasanii hao wakubwa Tanzania ni kama vile Mzee YUSUPH, BANANA ZORRO, FLORA MBASHA, ENIKA, CAROLA KNASHA NA THE WAHAPAHAPA BAND, ambao wote watatumbuiza katika jukwaa moja kuanzia saa saba mchana siku ya jumapili mchana june 7.
Muziki na mashairi yanayoendana sambamba katika kundi hili la wasanii wakubwa na maarufu Tanzania.Huku ukitoa ujumbe kadhaa kuanzia mawasiliano ya mzani-mtoto, unyanyapa, kutubu, tabia na kujali, kila nyimbo katika albamu hii imekaguliwa kwa uangalifu ili kuangaza uhalisi unaowakumba watanzania wanaoishi katika ulimwengu wa gonjwa la Ukimwi HIV.
Wahapahapa- tamthiliya ya kila wiki inayorushwa kila jumatatu kuanzia saa kumi na mbili jioni kupitia Radio Free Africa, Radio one na vituo vingine, hujishughulisha na muziki kama maigizo.Tathiliya hiyo inahusu wanamuziki chipukizi wanaojaribu kujikomboa kimaisha katika nyakati hizi za HIV/AIDS. Mradi huu umefanikishwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia United states Agency for international Development (USAID).
MSETO WAHAPAHAPA ni mchango wa muziki kutoka kwa baadhi ya wasanii watanzania .Kupitia midundo na mashairi, wakati hawa watanzania wenye vipaji wameweza kuteka mioyo na roho ya tamthilia ya wahapahapa katika hali ambayo watanzania hawajawahi kusika au kuona.
No comments:
Post a Comment