Friday, August 14, 2009

Adhabu ya miaka 30 jela, madereva wagoma wachelewesha safari za mikoani leo asububi!!!

Baadhi ya madereva na abiria wakiwa pembeni ya mabasi ya kwenda mikoani isivyo kawaida kwa mida km hiyo. Ambapo majamaa waliamua kugomea serikali adhabu waliyoiita ya uonevu dhidi ya madereva wenzao wa Tanga na Moshi waliyohukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kusababisha ajali iliyoua watu hivi karibuni.

Wao wanasema adhabu hiyo ni kubwa sana kulinganisha na ile ya sasa ya miaka 2 jela au faini ya shs. 30,000 hadi 300,000 ukizingatia kuwa ajali ni bahati mbaya wao pia hawapendagi zitokee!!!
Hata hivyo baada ya masaa kadhaa hivi safari zilianza kwa kuchelewa sana zikiacha baadhi ya abiria kutojua cha kufanya.

No comments:

Post a Comment