Tuesday, August 11, 2009

BSS YATANGAZA WALIOINGIA 10 BORA, VODA WAWAZAWADIA SIMU ZA MIKONONI!!!!

10 bora wa BSS 2009 wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.

Washiriki walioingia 10 bora mashindano ya BSS ni pamoja na Imani Lisu (Arusha), Beatrice William, Pascal Cassian (Mwanza), Mwapwani Yahaya, Sarafina Mshindo (Dodoma), Peter Msechu (Kigoma), Jackson George (Tanga), Catherine Ntepa, Kelvin Mbati na Mary Lucos (Dar es Salaam).

"Washiriki wa mikoani wameonekana kungara zaidi mwaka huu ambapo pia tumeona idadi ya washiriki sita kuwa wakinadada na washiriki wanne wakina kaka ambapo kwa kiasi kikubwa mwaka huu kuna mabadiliko makubwa ya kiushindani,"alisema Ritta mkurugenzi wa Benchmark.

Ritta alisema washiriki hao watatambulishwa rasmi jumapili ya wiki hii katika ukumbi wa Malaika ambapo wataimba wimbo wa pamoja walioutunga unaohusu masuala ya ukimwi.

No comments:

Post a Comment