moja kati ya mashindano ya kutafuta vikundi vya kuwakilisha mikoa ktk fainali za kitaifa itakayofanyika Diamond Jubilee
Prof Jize anatarajia kusindikiza fainali ya kitaifa ktk lile shindano la kushake la 'Malta Guinness Street Dance Afrika' itakayofanyika ijumaa hii katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Pamoja na mc huyo shupavu kutakuwa na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya km Chid Benz, Marlow, Mwasiti na C Pwaa.
Vikundi 10 vya kucheza muziki vitachuana kutafuta kikundi bora ambacho kitawakilisha TZ katika mashindano ya kimataifa yatakayofanyika Septemba 12 Nairobi. Ktk mashindano hayo mshindi ataibuka na kitita cha sh. Millioni 3 wa2 sh. millioni 2 na wa3 shs.millioni 1.
Vikundi vilivyoingia fainali ni Moro Squad - Morogoro, Contagious - Arusha, Saxers Group na Familia Bora vya Tanga, B2K Group na New Edition kutoka Mwanza, The Chocolate na Best Friend vya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment