Monday, August 10, 2009

STARZ YAKABIDHIWA BENDERA NA JEZI MPYA, KUKIPIGA NA RWANDA AGOSTI 12!!

Kaimu Mkurugenzi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Charles Matoke, akimkabidhi Bendera nahodha wa 'Taifa Stars', Salum Swedi leo jijini Dar.

Timu ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars' leo jioni inatarajiwa kuondoka kwenda nchini Rwanda, kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya nchi hiyo 'Amavubi', huku ikikabidhiwa uzi mpya wa timu ya taifa, ambao ndio utakua ukitumika katika mechi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment