Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Askofu Zachary Kakobe ameonyesha kutokubaliana na miongozo iliotolewa na viongozi wa dini juu ya uchaguzi ujao wa viongozi wa serikali. Makavu hayo alikuwa akiyaelekeza kwa maaskofu waliotoa waraka wa Kanisa Katoliki nchini na Mwongozo uliotolewa na Shura ya Maimamu akisema maandiko hayo ni hatari kwa amani ya Watanzania.
Alipokuwa akiongea na wana habari kanisani kwake jana, Askofu Kakobe alisema Uchaguzi Mkuu wa 2010 ni wa viongozi wa Serikali na kwamba viongozi wa dini hawana haja ya kutoa mwongozo kuhusu uchaguzi huo.
Askofu kakobe aliyevalia blue akifuatilia moja ya mikutano ya kisiasa mwaka jana
"Sisi kama maaskofu tunapaswa kuwa wadau wakubwa wa amani kwa kuheshimu mamlaka na falme zinazotawala dola ili tupate kuishi kwa amani," alisema.
"Wakati wa uzinduzi wa Mwongozo walikuwa wanasema wakatoliki wamemwaga ugali na sisi tutamwaga mboga, hii ni dalili ya kwamba nchi sasa itapasuka," alisema.
No comments:
Post a Comment