Wednesday, September 2, 2009

Vodacom Miss Tanzania 2009 yapata mdhamini mwingine!!

Mkurugenzi wa mashindano ya urembo Tanzania Hashimu Lundenga (kulia) akibadilishana mkataba wa udhamini wa mashindano ya Miss Tanzania na Meneja wa bia ya Redd's Kabula Nshimo jijini leo, katikati ni Meneja udhamini wa TBL, George Kavishe.

Bia ya Redd's premium imetoa udhamini wa sh. milioni 200 ktk kinyang'anyiro cha kumsaka mnyange wa Tanzania, akizungumza Dar es Salaam leo Meneja wa Redd's Kabula Nshimo alisema wao na Kampuni ya Lino wameingia mkataba wa miaka mi3 wa kuwa mdhamini mwenza wa mashindano hayo, pia Samsung ni mdhamini mwingine wa mashindano hayo yatakayofanyika Oktoba 2 mwaka huu pale Milimani City.

Alisema mashindano ya mwaka huu hayatakuwa na balozi wa Redd's isipokuwa kutakuwa na mashindano ya kumsaka Miss Photo Genic atakayepatikana kupitia issamichuzi.blogspot.com na kwamba mshindi huyo atafanya kazi anazotakiwa kufanya balozi wa Redd's.

No comments:

Post a Comment