Monday, September 7, 2009

Kwa hili nawapa BigUp COSOTA...!!

Chama kinachosimamia Haki Miliki za Wasanii Tanzania (COSOTA), kimesema hakitawaachia huru watuhumiwa saba waliokamatwa kwa kunakili kazi za wasanii mpaka watakapotoa vibali halali kutoka kwa wamiliki wa kazi hizo vinavyothibitisha kuwaruhusu kunakili kazi zao, ndipo watakapowafutia kesi inayowakabili ya kukutwa na kanda feki, na ikiwa hawatakuwa na vibali hivyo, wataendelea kuwa mikononi mwa polisi huku vitu walivyokutwa navyo, kuchomwa moto.

Watuhumiwa hao walikamatwa hivi karibuni katika operesheni ya kusaka kanda bandia iliyofanyika katika maeneo ya Kariakoo, Buguruni na Tabata jijini Dar es Salaam, ambao ni Ayaj Amash Chavda, Abass Adam Salehe, Kamugisha Shop, Ana Maria, Moses Msigwa, Kihiyo Athumani, James Mbelwa na Loveness Masonda, walikamtwa na VCD, DVD, VHS na vifaa vya kufyatulia kanda hizo vikiwa na jumla ya thamani ya sh.191,200,000.

" Tunajua matatizo haya kumalizika haraka ni vigumu kutokana na watu hao kuwa na mtandao mkubwa, lakini COSOTA tutahakikisha tunachuana nao na kukomesha kabisa," alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa (COSOTA), Lustus Mkinga.

No comments:

Post a Comment