World News

Monday, September 28, 2009

Akon kuperform tuzo za Mtv (Mamas) Kenya...


Mwanamuziki nguli wa Hip Hop kutoka nchini Marekani, Akon anatarajia kutoa burudani katika tuzo za muziki za MTV (MAMA) na Zain Oktober 10 mwaka huu jijini Nairob nchini Kenya.


Mwanamuziki huyo mwenye asili ya Senegal ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki atatumbuiza katika tuzo za MAMA 2009 akiwa sambamba mwanamuziki wa zamani wa kundi la Fugees, Wyclef Jean na wanamuziki mahiri kutoka Afrika wakiwamo Wahu, M.I., Samini and Lira.


Akon alisema amefurahi sana kusaini mkataba wa kutoa burudani katika tuzo hizo kwani anajihisi furaha zaidi anapo kuwa akitoa burudai katika nchi zilizo barani Afrika.
“Afrika ni moyo wangu. Najisikia kubarikiwa kuweza kutumbuiza nchini Kenya na ni heshima kwamba MTV na Zain waliniomba kuwa sehemu ya tukio hilo kubwa," alisema Akon.
Alisema, amejiandaa vizuri kwa kutoa burudani diku hiyo ambapo atatumbuiza kwa nyimbo zake binafsi na kuimba sambamba na Wyclef katika nyimbo alizomshirikisha.


Akon ambaye pia ni mjasiriamali na mhisani, amekuwa akitamba duniani tangu aingie katika ulimwengu wa muziki kwa mara ya kwanza mwaka 2004 na albam yake ya kwanza ya “Trouble” iliyoshika namba moja katika chati za Billboards ambapo kwa sasa amejikita kwa kusaidia vijana waliokosa fursa katika nyanja ya muziki.


Sambamba na kusaidia vijana pia ni mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa lebo mbili za kurekodi za Konvict Muzik, ambayo imetayarisha muziki wa wasaniib kama T-Pain na Asher Roth.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...