World News

Tuesday, September 29, 2009

DULLAYO AKAMILISHA 'NAUMIA ROHO' VIDEO..!

Msanii wa Bongofleva Dullayo aka D Timing amekamilisha Video ya nyimbo yake mpya "Naumia Roho" iliyopigwa mkono na ABRAH 'Tha Producer' chini ya kampuni yake inayokuja juu kwa sana hivi sasa ya GHS, kabla ya video ya Dullayo mchizi alishapiga mikono ktk Video nyingi sana hapa Bongo hasa alipokuwa na kampuni ya Visaual Lab. kwa Adam Juma.

Moja ya video iliyomvutia Dullayo mpaka akaamua kupiga na Abrah ni ile kazi ya msanii anayeitwa 'Tox star', Hii inakuwa video ya kwanza kabisa kwa msanii Dullayo tangu alipoanza kutoka ktk medani hii ya bongofleva na album yake ya IMANI yenye nyimbo 10 km Bila yule, Nipumzishe, Muda bado, na Makavulive ambazo tayari zimeachiwa. Nyimbo nyingine ni Mwanzo mwisho, Maswali, Imani, Sifikirii, Leo, na Uwe wangu.

Akiwa mbioni kukamilisha album ya 2 itakayoitwa MAISHA SIO SINEMA, Dullayo amesema atajitahidi kila ngoma atakayokuwa anaachia aipigie video ili wananchi wasiishie kumskiza tu kwa audio wamuone na anavyong'ara pia.

Ktk Video ya Naumia Roho Dullayo amefanya na mabinti wa2 wakali, mmoja aliyefanyanae zaidi anaitwa Esta ambaye pia ni mcheza filamu chipukizi bongo, ambapo Dullayo alimuona baada ya kufanya vizuri ktk filamu ya 'Its too late' aliyocheza na Yusuph Mlela. Yupo mnyamwezi ambaye nae amefanya vizuri sana ktk video hasa kipande ya story ya mapenzi alichocheza na Esta, mchizi anaitwa Chingy Bling 'mzee wa kuuza'. Pia wapo washkaji kibao ambao ni wasanii wanaorepresent crew ambayo pia Dullayo nae yumo ya Makavulive, hapo namzungumzia Ommy G, Xdizo, na Eazy man.

Fanya uitazame mdau, halafu tutoe maoni tuone, imekuwaje...!?

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...