World News

Friday, September 25, 2009

Warembo wa 'Miss Vodacom Tanzania 2009' wapigwa shule ya UTALII...!Warembo 30 wanaoshiriki Miss Vodacom 2009 wamepatiwa semina juu ya utalii ili kuongeza ufahamu juu ya utalii wa ndani.Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB, Geofrey Meena alisema jana kuwa lengo la semina hiyo ni kuhakikisha mrembo atakayetwaa taji la Miss Utalii wa ndani atangaze vyema utalii huo ili awe balozi mzuri kwa nchi yake."Kabla hatujawauliza maswali siku ya mashindano, tumeona tuanze kwanza na semina hii ili waweze kujibu maswali yetu kwa ufasaha, kupitia warembo hawa tunaimani tutatoa balozi mzuri atakayeitangaza nchi kupitia vivutio vya ndani,'alisema Meena.Meena alisema balozi wa Utalii wa ndani Miss Utalii atapatikana katika warembo watakaoingia tano bora za kinyang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania 'Vodacom Miss Tanzania 2009' mnyange atakayetwaa taji hilo ni yule atakayejibu kwa ufasaha maswali yanayohusu utalii wa ndani na kwamba maswali watakayoulizwa siku ya kinyang'anyiro hicho yatatokana na semina hiyo.Mnyange atakayeibuka kidedea katika kinyang'anyiro hicho cha kumsaka Miss Utalii wa ndani ataibuka na zawadi zenye thamani ya sh. milioni 3.3.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...