World News

Friday, October 9, 2009

TID kutambulisha album yake "Prison Voice" Club Billicanas Oktoba 11...!!

Meneja masoko wa Bilicanas, Anton Kizito (kushoto) na TID (kulia), wameingia mkataba na TID na bendi yake ya Top Band kufanya onyesho kila siku ya Jumapili kwa muda wa mwezi mmoja.


Mwanamuziki wa kizazi kipya, Khalid Mohammed ‘TID’,ambaye hizi majuzi ameshinda Tuzo ya KISIMA Video of the Year Tanzania anatarajia kuzindua albamu yake inayokwenda kwa jina la ‘Prison Voice’ Oktoba 11 Jumapili hii, ndani ya ukumbi wa Bilicanas.

Akizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi huo, TID ameinadi albamu hiyo kwa kusema kuwa itakuwa bora kuliko zile alizowahi kuzitoa.

Alisema albamu hiyo inazungumzia hali halisi pamoja na maumivu yote aliyoyapata wakati alipokuwa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kutokana na kosa la utovu wa nidhamu.
Albamu hiyo itakuwa na nyimbo 12 ambazo baadhi yake ni kama ‘Asha’ (uliobeba jina la albamu na kutamba katika vituo mbalimbali vya redio na TV), ‘Siwezi’, ‘Tupendane’ na ‘Only One’ ambao ameurekodi nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...