World News

Thursday, November 26, 2009

Tamasha la 'Save Albino' lafana Marekani....!

Albino Fulani kulia akiwa na Chino msanii wa Zambia wakiwaburudisha wadau waliohudhuria ktk tamasha la Save Albino benefit lililofanyika jmosi iliyopita huko Columbus Ohio Marekani.

Tamasha hilo liliandaliwa na Msanii huyo Mtanzania Babu Sinare aka 'Albino Fulani' anayeishi nchini Marekani kwa lengo kuu la kuwasaidia ma-albino waishio Tanzania. Tamasha lilihudhuriwa na watu wengi na kutumbuizwa na wasanii wengine kutoka Zambia na Kenya.
Mapato ya tamasha hilo yalinunua mafuta ya kinga ya ngozi kwa watoto ambayo yalitolewa kwa bei ndogo na kampuni ya Walgreen ya huko Marekani na yanatarajiwa kukabidhiwa kwa chama cha Maalbino nchini Tanzania hivi karibuni.Baadhi ya wadau wakishangilia show kutoka tamasha hilo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...