World News

Thursday, January 7, 2010

Pamoja na kutufunga majuzi.... JK afurahishwa na Didier Drogba!!


Rais JK akimkabidhi Didie jezi ya Taifa stars yenye jina lake mgongoni, pia aliwakabidhi km Eboue, Toure, Kaluo na wengine

Rais Kikwete amekunwa na kauli iliyotolewa na mshambuliaji hatari wa timu ya Taifa ya Ivory Coast 'The Elephants' na Chelsea ya Uingereza, Didier DROGBA baada ya kuzungumza vizuri na vyombo vya habari vya Kimataifa akiisifia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa stars'.

Makepteni wa timu za Taifa Nsajigwa shoto na Drogba kulia siku walipocheza mechi ya kirafika na Drogba kuifungia timu yake goli 1 bila majibu.

'Ivory Coast ni timu kubwa Afrika tena ni ya kwanza katika ubora wa viwango katika ukanda wetu, hivyo kukubali kucheza na Tanzania ambayo ni nchi changa katika soka ni fahari na heshima kubwa sana kwetu,'' alisema Kikwete.

''Drogba alizungumza vizuri sana alipohojiwa na Skysports ambapo aliisifia sana Tanzania kwani hakutarajia kama wangepata ushindani mkubwa kama ule ambapo alisema Tanzania ilicheza kwa ushirikiano, walishambulia bila woga kwa pamoja,'' alisema Kikwete ktk hafla ya chakula aliyowaandalia wachezaji wa Ivory coast, Taifa stars na Amavubi ya Rwanda.

''Kutokana na kauli hiyo ana imani Drogba atakuwa amefungua milango kwa timu kubwa zingine kuja nchini kucheza na timu yetu ya Taifa ambapo pia kupitia Drogba Dunia nzima imefahamu Tanzania ina kiwango gani cha soka,''.

Mrisho Ngasa mshambuliaji machachari wa Yanga na timu ya Taifa stars akitulizwa na beki wa Ivory coast Guy Demel amaye pia anachezea timu ya SV Hamburg ya Ujerumani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...