Monday, February 15, 2010

Bi Kidude alikacha Tamasha la Sauti za Busara kupiga tafu vita ya Malaria Tamasha la ZINDUKA..!


Bi Kidude akisalimiana na Rais Kikwete ktk tamasha la ZINDUKA lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar tarehe 13 February mwisho mwa wiki

kikundi cha Tausi Women's Taarab cha Zanzibar

Fatuma binti Baraka aka Bi Kidude msanii mkongwe na mahiri mwenye heshima nyingi ktk muziki wa Taarab Tanzania alitegemewa kuperform na kikundi cha Tausi Women's Taarab ktk Tamasha kubwa la kila mwaka la SAUTI ZA BUSARA linalofanyikaga Zanzibar, ila alikacha tamasha hilo na kushiriki ktk tamasha jingine lililokuwa na lengo kuu la kupinga vita ugojwa wa Malaria la "ZINDUKA" ambalo Raisi Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi na kuungana na wanamuziki na wasanii wengine ktk kupinga Malaria Tanzania.

Tamasha la ZINDUKA lilifanyika siku moja ya tarehe 13, ambapo pia siku hio Bi Kidude alitakiwa kuperform ktk Tamasha la SAUTI ZA BUSARA saa 1 za jioni akiwa na kikundi cha Taarab cha Zanzibar kinachoitwa Tausi Women's Taarab.


No comments:

Post a Comment