Wednesday, August 4, 2010

Ukiwahi kuingia Fiesta keshokutwa GAMBE bureee..!


Kampuni ya bia ya Serengeti imetamka rasmi leo asubuhi kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM 88.4, kuwa itatoa vinywaji vyake bure kwa watu wa kwanza watakowahi kuingia kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,linalofanyika ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijin Dar .

Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii wa kampuni ya Bia ya Serengeti ,Teddy Mapunda (pichani kushoto) ameweka hilo bayana ndani ya kipindi hicho leo asubuhi kuwa ,watu watakaofika ndani ya tamasha hilo kabla ya saa 12 jioni watapewa bia moja ya bure,na watakaofaidika zaidi ni wale wenye umri zaidi ya 18.

Teddy amesema kuwa kutokana na Familia ya kampuni hiyo kuwa kubwa,washabiki na wapenzi wake watakuwa na uhuru wa kuchagua bia waitakayo,kwani zitatolewa bia za aina tatu,yaani bia ya Uhuru,Tusker pamoja na Serengeti a.k.a Mfalme wa raha kamili.

Kampuni ya bia ya Serengeti ndio mdhamini mkuu wa tamasha la Fiesta Jipanguse 2010.

No comments:

Post a Comment