Msanii Dullayo ameripoti kunusulika ktk ajali mbaya aliyoipata hivi karibuni akiwa ktk pilika za kufanya PA huko Korogwe Tanga ikiwa ni ktk show aliyoandaliwa na mapromota wa huko....
Akielezea jinsi ilivyotokea D-Timing kama anavyopenda kuji-introduce alisema alikuwa ktk gari iliyobeba spika kubwa kadhaa na jamaa mwingine nyuma ya gari huku wakiendelea kutangaza uwepo wa show hio ambapo yeye ndio alikuwa sterling wa hio show gafla dereva akitaka kukata kona gari hio ilipinduka wao na ma-spika huko nyuma wote wakaenda chini.... alipopata fahamu alijikuta akiwa mbele ya gari karibu na dereva ameshikiliwa kuelekea sehemu ya huduma ya kwanza!
Kwa sasa jamaa anaonekana yuko vizuri huku akiendelea kuuguza majeraha madogo na mguu ambao bado umevimba kdg
Pole mnyamwezi kwa yaliyokukuta! Tha saga continue......
No comments:
Post a Comment