Verse 1
Welcome to Ukonga wakazi ninapotoka/
Nilipokulia pia kujifunzia kufoka/
Bonde la mto msimbazi im chillin with Red Scouts/
Tuna rap an ku blaze yeaaaaaah that’s right/
Nachukua fursa hii kuwaeleza wasio kufahamu/
UK kitongoji cha jiji la Dar es salaamu/
Wazee wa gambe tunaanzia Hill-tech/
Malipo fedha taslimu, kadi mpaka check/
Wazee wa safari uwanja wa ndege upo kwetu/
Hata safari kafiri bila begi au peku/
Lango la jeshi ni pembeni ya majumba sita/
Sokoni kwa wale ambao wanaopenda kupikapika/
Na wenye nguvu zao bado wanaweza kulima/
full ma diko diko pamoja na mabang’abing’a/
wingi wa watu wengi wanakaa gongo la mboto/
haswa wazawa wa mkoa wa mara si kitoto/
ukija stakishari kama si mnyakyusa, mchaga/
hivyo kutwa nzima ka si shimboni, ni ndaga/
relini, kitunda, banana na saba saba/
mwisho wa lami, kanisani, magereza na Mombasa/
minazi mirefu, mogo pamoja na karakata/
airport, black people nacho chochote utapata/
Taxi bubu, mifugo, bar ndio biashara/
Kila mtu full shangwe hata wasio na mishahara/
Ukiniona kwa mbali unaweza kusema wakishua/
Na nisipo kuhadithia napotoka huwezi kujua/
Msaada njia panda ya segerea ukiweza kuminya/
Chorus
Welcome to Ukonga where we don’t play/
Machizi wanajichanganya like everyday/
Kimuziki na mabinti dar nzima haituoni/
And parties don’t stop till 8 in the morning/
Verse 2
Nimezaliwa mjini, kukulia uswahilini/
Hivyo anayejua maisha ya aina yote ni mimi/
Tofauti na UK nchini Uingereza/
Uk yetu sisi ina mawili magereza/
Uhalifu hauishi hata maisha wakipoteza/
Kujipitisha vichochoroni usiku unacheza/
Majambazi sura zao zinafanana na mimi/
Hivyo si hatari ukisikia nimelala mabatini/
Kalamu zimeisha wino R.B haziandikiki/
Polisi hata wakivaa kanzu, waalifu hawashikiki/
Hebu tuweke kando, hebu turudi kwa mabinti/
Watoto wote kiwango, hakuna ambaye halipi/
Ina kuwanasa wewe lazima uwe fiti/
Bila yai, mishikaki, kuku, chipsi haziliki/
Wengine usiku hauendi bila ya beer baridi/
Utawakuta kwa mramba, bar mpya au kwa Daudi/
Ukonga nayo haipo nyuma kwa mastaa/
Wamezaliwa nyota wengi katika hivi vitaa/
Caz T, Nkurumah, pamoja na Shabobo/
Peter Njovu, Lugano, marco Chali pia na Obo/
Dullayo, Gie manie, Esther na kadhalika/
Wauza sura kibao utawakuta kwa Kabalika/
Majina yamenitoka wala hamja sahaulika/
Hivyo kama tupo pamoja, pamoja tunawakilisha/
Black Messenger, Wile Mavisu, Tarik the rebel, Devi, Simbano, Luse, Amani, Wema, Nono, Makwala, D knob, Soggy doggy, hotpot family, kwa mwasandende, kwa mwakyusa, ngwilulupi, apio, kwa mwakipesile boni, maka, u know everybody in the house man
Baraka Elias mashauri, whats up tolu….
No comments:
Post a Comment