World News

Wednesday, April 20, 2011

Q Jay ahamia kwenye maPambio...!


Joseph Mapunda aka 'Q - Jay' amesema kwasasa ameachana na muziki wa Bongoflava na badala yake ataanza kuimba nyimbo za kumsifu Mungu,
mchizi amesema ameamua kuimba nyimbo hizo na kuokoka ili aweze kuachana na matendo maovu ambayo hayana maana ktk maisha yake.

Amesema muziki aliokuwa akifanya ni wa kidunia na amewashauri wasanii wenzake wote wanaoimba nyimbo hizo waache ili waweze kumsifu Mungu kwa nyimbo za mapambio.

Kwasasa amepumzikiza kufanya muziki mpaka mwezi Juni atakapoanza kurekodi nyimbo za kumsifu Mungu pekee sambamba na kutoa albamu yake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...