World News

Friday, January 6, 2012

Mwandishi FRANSIS GODWIN, kuwafundisha WASANII wababe!!DIAMOND akiwa anaingia kwenye hiyo show siku ya tukio la kumshambulia 'paparazi' ambapo inadaiwa alichelewa.


staa wa muziki Bongo, DIAMOND PLATNUMS kupandishwa mahakamani jumatatu mjini Iringa, kwa tuhuma za kumshambulia mwandishi wa habari Francis Godwin, na kuonyesha kumpuuza. (ameandika Godwin kwenye blog yake)


mwandishi huyo anaedai kupigwa na kuvunjiwa CAMERA na msanii DIAMOND PLATNUMS wiki iliyopita katika uwanja wa SAMORA, alisema amekataa kupokea pesa alizopewa na DIAMOND, na kusisitiza kwamba yeye hana shida ya pesa, anachotaka ni DIAMOND KUMUOMBA MSAMAHA.

mwandishi Francis Godwin amesema ndugu na jamaa wa karibu wa DIAMOND wamekua wakifanya jitihada za kumpatanisha ili swala hilo liishe, ambapo juzi mwandishi huyo na mdhamini wa DIAMOND Edo Bashir walitakiwa kwenda kwenye kituo cha polisi, ambapo mdhamini huyo alikiri kwamba DIAMOND amekubali kulimaliza hilo swala nje ya kituo cha polisi.

Mwandishi huyo amesema Edo (mdhamini wa DIAMOND) alisema Diamond amekubali kulipa gharama za uharibifu kwa mwandishi huyo ambazo zilikua ni MILIONI MOJA na LAKI NANE, ambapo waliomba kupunguziwa iwe MILIONI MOJA NA LAKI SABA.

walipofika Polisi kukabidhiana hizo pesa, mwandishi huyo alimuuliza EDO, “unasema tumalize hili swala lakini mpaka sasa sijapokea simu kutoka kwa DIAMOND au ndugu yake yoyote hata wakinijulia hali, na wewe unasema unawasiliana nao, kwa hiyo ameona wewe ni BORA kuliko mimi, nikamwambia SAMAHANI kwa mazingira haya, kwa sasa siko tayari kulimaliza hili swala” – Francis.


baada ya hapo Askari alimwambia mwandishi huyo aite mashahidi wake, na akafanya hivyo, ambapo Francis anasema


"nimeitwa tena polisi na kuulizwa msimamo wangu, nikawajibu DIAMOND ameona ni haki yake kunipiga na kuvunja vifaa vyangu, swala hili mimi naomba liende mbele, twende MAHAKAMANI kwa sababu lengo langu sio kutaka hela za DIAMOND, ni UTU wangu kwa sababu sisi waandishi wa habari tumeendelea kunyanyasika na KUSAMEHE, lakini hili la DIAMOND nataka iwe fundisho na kwa wasanii wengine” amemalizia FRANCIS GODWIN


Kwa Msaada wa MillardAyo/gongamx.
No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...