Waziri wa afya na ustawi wa jamii wa Jamuhuri ya muungano Mhe.Bw.Seif Rashid na waziri wa afya wa Zanzibar Mhe. Rashid Seif Suleiman, Siku
ya jumapili 25 januari 2015 (jana) walikutana na kuongea na baadhi ya
watanzania waishio nchini ujerumani katika hoteli ya Martim Hotel mjini
Berlin.
waziri wa afya mhe.Seif Rashid (mwenye miwani) akiteta na watanzania ujerumani,mwenye kofia mwanamuziki Ebrahim Makunnja aka kamanda Ras makunja |
Mawaziri hao kwa pamoja waliongozana na balozi Tanzania nchini
Ujerumani mheshimiwa Bw.Philip Malmo,katika mkutano huo mawaziri hao
wote walielezea jinsi wizara zao zinavyofanya kazi kuhakikisha kuwa
huduma za afya zinawafakia walio wengi na pia kuhakikisha siku za usoni
kila mtanzania atatanufahika na uduma hizo kwa kutumia bima ya afya bila
kujali tofouti za uwezo wa vipato vyao.
Watanzania waishio ujerumani
wamefarajika sana na mkutano huo,pia mawaziri wamewataka watanzania
waishio ughaibuni kuchangia kuwekeza
katika
sekta ya huduma ya afya hata ikiwa ni sekta binafsi ,mawaziri hao
wamesema milango ya wizara zao hipo wazi kwa watanzania wanaotaka
ushauri,ushirikiano au kuwekeza katika sekta hizo.
No comments:
Post a Comment