Thursday, October 31, 2013

Steve RnB KuPerform @'Welkom Back Party' na Wanachuo!

Ndani Ya Ambassadors Lounge “Ijumaa Hii”Ya Tarehe 01.11.2013 Itakuwa Ni Kuua Ndege Wawili Kwa Jiwe Moja
Ni “Welcome Back Party” Ya Wanafunzi Wote Wa IFM Ambao Mlikuwa Likizo Na Sasa Mmerejea Chuoni
Na Pia Ni “Welcome Back Party” Ya Msanii STEVE RNB Ambae Kwa Muda Mrefu Sasa Hujamsikia Wala Kumuona Sababu Alikuwa Kwenye Tour Ndefu Nje Ya Nchi,Njoo Umuone Akiperform Hit Single “Jambo Jambo” Na Akitambulisha Wimbo Wake Mpya “Huyu Demu” Feat Mr Blue
Kama Kawa Kwenye Decks Ni Dj Steve B/Dj Skills Along Side Dj Pac Na Dj Masu
Kiingilio NI sh 10,000 tu mlangoni kuanzia saa 3 usiku
Wanafunzi Wa Vyuo Vyote Vingine Vya Dar-es-salaam Mnakaribishwa Tujumuike Kwa Pamoja... Sana Tu

Tuesday, October 29, 2013

Pole sana Wema.......Rest in Peace Mzee Sepetu!



Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria msiba wa Balozi Abrahamu Sepetu (Baba mzazi wa Wema Sepetu) uliotokea hapo juzi jijini Dar es Salaam.
 
Mheshimiwa kiwete amefika msibani akiongozana na mkewe hapo kutoa pole kwa familia hiyo kwa  kuondokewa na Balozi Sepetu ambaye hapo alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye serikali nchini ikiwemo ya kuwa waziri wa mambo ya nje kwenye miaka ya sabini (70) kabla  ya kuwa balozi wa urusi kwenye kipindi cha miaka ya 80. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

BAC-T Release "PAMOJA NA SISI" in featuring with TRU D

Bac-T Release "PAMOJA NA SISI" feat Tru-D. This is the 2rd single from the album “REALITY CHECK”  this album will come out by the end of this year 2013. It’s that album which is full of  Hip Hop flava and talks about realities of life in our East African Societies.

The song is written by Bac-t together with True-D and was produced and mixed by Jay-P – HOPE STREET STUDIOS  – KIGALI, RWANDA

For more details conflict: +250788781609

G-Hood ft Defxtro-Naendelea Kutafuta

Rapper G-hood anayewakilisha pande za Usa River Arusha anadrop full package ya wimbo wake "Naendelea Kutafuta" Noizmekah Production na video chini ya Paradise Videoz Usa River kazi yake director Hussein,pata kusikiliza audio HAPA na Video HD Quality HAPA, kwa mawasiliano/mahojiano zaidi check nae kwa simu nambari +255 759 903 824 powered by www.vmgafrica.com
--
Official Audio G-Hood ft DefXtro-Naendelea Kutafuta http://goo.gl/eiK9kI

CHUMA cha MOTO kutoka kwa Willy Fololo & Ghetto Grade

Chumaliet au "Chuma Cha Moto" ni brand new ngoma toka kwa wakali wa Dancehall Willy Fololo pamoja na Ghetto Grade" CHUMALIET/LEO ikiwa ni audio na Video toka Noizmekah HoodPixx Arachuga chini ya Defxtro, Pata kudownload wimbo kamili HAPA na Video hapo chini, kwa mawasiliano zaidi check nao kupitia +255 656 477 793 na +255 757 435 609 powered by www.vmgafrica.com
--
WillyFololo & GhettoGrade-Chumaliet  http://goo.gl/ucoeFc
Video http://youtu.be/Pi89VPPYPBM

Warriors from the East ni "NOMA", Official Release

Official release ya Video + Audio ya reggae dancehall toka kwa washindi wa tuzo za reggae 2012/13 "Warriors From The East", Ngoma ikiwa inakwenda kwa jina "Kaskazini Noma" tazama
na pia sikiliza/download official audio yake HAPA kwa mawasiliano zaidi check na warriors kupitia +255 765 789 373 au +255 784 152 766 powered by www.vmgafrica.com
Warriors From The East-Kaskazini Noma [Audio]  http://goo.gl/pvazFz

New Sound; BATA - Seminde ft Mubbyzow

Song: Bata
Artist: SEMINDE ft. MUBBYZOW
Produced byL Mubbyzow

Audio Link:
http://www.hulkshare.com/mchomo/seminde-ft-mubbyzow-bata-1

Friday, October 25, 2013

"TIME" ZA P-CULTURE

Anakuja P-culture na Ngoma "Time" toka pande za Arachuga, ikiwa ni ngoma toka kwa producer Defxtro mahadhi ya Dancehall Ragga, download na sikiliza HAPA na kwa mahojiano/Mawasiliano zaidi check na P-Culture kwa simu nambari +255 782 123 700 powered by www.vmgafrica
--
Mwanadada P-Culture na Time http://goo.gl/4t49YN

Muder Plus Lyrics - Chaba ft. Jordan

Ikiwa bado mixtape yake “Nyota njema ya mtaa” inaendelea kufanya vizuri sokoni, Chaba a.k.a Baba mkubwa anayewakilisha 009 (Ngalimited) Arusha city, anawazawadia wapenzi wa muziki wake track mpya na moto kabisa toka Grandmaster Records chini ya utayarishaji wa producer John B akiwa amemshirikisha Jordan aliyetisha na ngoma yake ya mapenzi vita mapema mwaka huu.
Huyu hapa ni Chaba akiizungumzia track yake mpya;- “Mmmmh! Hii track basically, ni zawadi kwa mashabiki zangu kwa kuipokea vizuri na kuinunua mixtape yangu ili pia wasio nazo waendelee kuinunua, na pia bila kusahau kuwa kawa bado Baba mkubwa nawa-murder rappers wote wanaoigiza sanaa”



For Interviews/Bookings; +255713876299


 Lyrics


Track; Murder
Artists; Chaba feat Jordan
Prod;   John B (Grandmaster Records)

Intro;- Kwa hiyo wee ndio jamaa wanamwita akachaba, Mmmmh! Ni nii special kuhusu we jamaa haah! Nini special, well mi nilikuja hapa kuwa-murder!!!!

Verse 1;-

Mistari mara Chaba sawasawa na mchongo,
Ule ambao ukijumlisha wenye akili ubongo,
Basi, unapata jumla ya cash milima, Mgosi wa ndima,
Mama kutoka Meru, Arusha nimesimama juu kuliko Meru,
Balozi wa Rap kutoka mashariki ya Africa, Sihitaji malaika,
Kunilinda kitaa, Nipo na mistari ambayo nikiigawanya haukatiki umeme mitaa,   
Una wivu sababu, Mistari yangu mara doo sawasawa na adhabu,
Kwa yako Career, Wewe ni umbwa unayelia, Nisipokuwepo nikiwepo unafyata mkia,
Basi, Jifunze kuiheshimu yako nafasi,
Huu ni urefu wa kamba hufikii kwa yako kasi, Najumlisha wafuasi,
Nikiwa-murder, Waigiza Hip Hop nakiwazika bila mashada,
Mi ni crazy Baba, Ndoto inayokukata stimu ya miaka saba,
Public figure linalochora miraba,
Isiyohesabika kama pundamilia wote wa Africa na yao miraba,
Unabakia historia kama Nebukalneza, Huu ni muziki wenye sura haijapendeza,
Kama mitaa ambayo serikali imeitelekeza,
Rasmi nipo hapa kuwala MC kama supu ya Pweza!

Chorus x 2 Nakubana tuu kwapani, Kwako nastay,
Nakutia shakani, Naku-murder everyway! Everyway!!
Bridge x 2 Nimechafukwa na roho na hawa mabishoo, Kuja na maswaga kwa Hip Hop show!! Tunawa-murder, (Murder)

Monster Muziq

As you know I've been heavy in the tees bizness for a while now, which by God's grace has enabled me the freedom and resources to pursue my real passion - music. I've been trying my hand at production for a while now with a new artist who's just released his promo debut single. I'd really appreciate some honest feedback on the potential of these two tracks.

You guys have the pulse of the industry at your fingertips literally, so your opinion will matter to me and my label. So please find the time to let me know what you think. Be brutally honest and if you like it hit me back for the 3-piece.

Azma WANASUBIRI NIFE (Official Music Video) HD

PROF JIIZE KUUZA "The Best of Prof. Jay" kimataifa

Profesa Jay akionyesha kwa wanaandishi wa habari (hawapo pichani) mfano wa hundi/bango alilokabidhiwa likiwa na Barcode kwa Bidhaa yake.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay.

Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya Barcode.
 
Hayo yamesemwa leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa akikabidhiwa Barcode za ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The Best of Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo zime heat tangu kuanza kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka kufanya vitu kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie watu wengi zaidi” alisema Jay.
 
Akiongea katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa Tanznia kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ya kwenye mtandao kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana Mmari alisema kuwa kwa kutumia fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni makubwa duniani kama CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya kwenye mtandao kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.
 
Aidha Mwenyekiti Mmari alitanabaisha kuwa wanamuziki wa Tanzania hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. Naye Afisa muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao haziko kwenye mfumo rasmi, “ukiangalia mwanamuziki kama Lady Jay Dee mathalani ana wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kama atatangaza kuuza kazi zake kwenye mitandao hiyo ni wazi atawafiukia washabiki wake kirahisi zaidi” Takwimu za Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji na mauzo ya kazi za mwanamuziki ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama Diamond ambaye kwa sasa ana mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona kupata takwimu sahihi za usambazaji wake.
 
Aidha amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo tunawaumiza wanamuziki na tunakuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. GS1 Tanzania ndio watoaji pekee wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania, ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza kwenye Supermarket na masoko ya mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za mistari yaani Barcode.

Tuesday, October 15, 2013

Usiku wa Dullayo @SWISS PUB Ijumaa hii!

Lets BOOGIE FRIDAY...............@Swiss Pub
Entrace fee 5,000/=

VMG Artist Publishing OFFER

Follow @vmgafrica on twitter & get Exclusive Release za wasanii wa Arusha na pia Muziki wa Bara la Afrika FaceBook VMG Africa for instant & Daily Infotainment updates from the African Entertainment Scene

Interested Artists Submit your Songs+Bio+Photos to "news@vmgafrica.com" for online publishing today, All Songs must be in form of Internet Links (Hulkshare/reverbnation/itunes/soundcloud) and photos (jpeg/png) 500x500 Pixels..other unlisted formats will be disregarded

Cultural Revolution waachia "Tabia yako"

Wanaitwa Cultural Revolution na wimbo wao unakwenda kwa jina Tabia Yako  ikiwa ni mkono wa Producer DizzoOne na vocal zimefanywa Noizmekah Studios, Sikiliza/Download HAPA na kwa mawasiliano zaidi check nao kuptia +255 767 554 041 na +255 763 050 787 powered by www.vmgafrica.com
--
Cultural Revolution-Tabia Yako (DizzoOne.Noiz) http://goo.gl/nVLlIA

Wazalendo na "Uzalendo" kutoka Noizmekah

"Uzalendo" toka kwa ToxicMan pamoja na KingTeja wakiunda Movement mpya "Wazalendo', ni ngoma inayodrop kwa mtindo wa HipHop Bounce, mkono toka Noizmekah Studio, Sikiliza/download uzalendo HAPA na kwa mawasiliano/Mahojiano zaidi check na wazalendo crew  kupitia +255 752 742 598 na +255 753 108 478 powered vy www.vmgafrica.com
--
Wazalendo-Uzalendo http://goo.gl/RSCVpk

Mixtape "Kaburi la Fisadi" ya Kabuku Digital iko mbioni kutoka!

Ikiwa imebakia miezi mitatu tuu kwa rapa machachari Kapuku digital aka mitishamba boy aka Bullet Proof kuachia Mixtape yake hii hapa ngoma nyingine itakayo patikana ndani ya mixtape hiyo ya KABURI LA FISADI isikilize alafu upime mwelekeo wa mixtape….balaaaaaaa..

Jackal Family waiachia "Harakati"

Wanaitwa Jackal Family, Hiphop artists toka Arusha wakiwa na Tumsime katika "HARAKATI" ikiwa ni ngoma toka Noizmekah Studios Arusha, pata kuisikiliza/Download HAPA na kwa mawasiliano/Mahojiano zaidi check na +255 784 809 585 powered by www.vmgafrica.com
--
Jackal Family ft Tumsime-Harakati http://goo.gl/XMueLA