Friday, July 30, 2010

CD ya "JAKAYA KIKWETE 2010" IMEINGIA NCHINI KWA KISHINDO KIKUBWA....!


Singo CD "Jakaya Kikwete 2010" kutoka kwao "Ngoma Africa Band"
IMESHATUA NCHINI KWA KISHINDO NA NGUVU ZAIDI !!!

PATA KOPI YA CD KWA KWA ANKAL MICHUZI

Hayawi !Hayawi ! Yamekuwa hile CD inayozungumziwa na washabiki wengi kila kona duniani
Sasa imeshatua nchini ,CD hiyo yenye jina "JAKAYA KIKWETE 2010" Kutoka kwao
"The Ngoma Africa Band" yenye maskani yake uko Ujerumani,Sasa unaweza kupata kopi za CD
hiyo kwa ANKAL Muhidin Issa Michuzi aka Mzee wa Libeneke,kwa simu 0754271266 wa blog ya
ya kimataifa ya jamii.


Pia kwa yeyote yule anayetaka atumiwe mp 3 au kuweka nyimbo hizo katika mlio wa Simu za viganjani
tafadhali usisite kuwasiliana na Ankal Michuzi kwa simu namba 0754271266 CD hiyo yenye mziki mtamu
unaosindikiza ujumbe muhimu kwa watanzania zaidi ya milioni 40 sasa CD hiyo ipo nchini na unaweza kupata kopi yake kwa kupiga katika sherehe ,mitaani,katika biashara yako,ndani ya mabasi,harusini,sokoni n.k
hili upate raha na ujumbe uliomo katika CD "Jakaya Kikwete 2010" utunzi wake Ebrahim Makunja aka
kamanda Ras Makunja wa FFU wa Ngoma Africa Band.


pia Jumamosi ya 31-07-2010 saa 4 hasubui Ras Makunja atahojiwa na radio Free Africa ya mwanza


tafadhali tega sikio.

Wednesday, July 28, 2010

KIDUM asema hana Bifu na Hermy B..!




Baadhi ya wadau wamekuwa wakiripoti kuwa Kidum msanii kutoka Burundi huenda akawa na bifu na producer wa Tanzania Hermy B kwa kuwa tu eti Kidum alifanya nae hit song Nitafanya na badae kufuta na kurekodi upya kwa producer mwingine aitwaye R KAY na kuipiga marufuku ngoma hiyo iliyofanywa na Hermy isichezwe kabisa kwa redio kitu ambacho ni kweli, akisema ngoma haina ubora





Lakini Kidum mwenyewe alikiambia kituo cha Kiss TV’s Hotsource that he has no beef and he re-recorded the song because he was not satisfied with the audio quality. Adding, the song was actually originally set to feature model turned singer K-lynn but she was away from the country at the time.


Ngoma bado iko juu ktk charts za bongo na kwingineko ikiwa kwenye collabo ileile ya Jay dee na Radios nyingi za Bongo zikiendelea kugonga ile version iliyofanywa na Hermy B version iliyofanywa na R KAY inatumika kwenye Video tu.

Tatiana amkaanga Mganda Big brother all star....!





Sammi, Uti na Tatiana, ni washiriki ambao wamepigiwa kura nyingi na wenzao za kutaka kutolewa kwenye jumba la Big Brother Africa.


Tatiana ambaye ndio Head of tha house, ana nafasi ya kujiokoa katika kupigiwa kura na kumpendekeza mwingine badala yake.


Mshiriki huyo alijitoa na kuweka Hannington katika kura za kutolewa Jumapili.


Sababu kubwa ya kumwingiza Mganda huyo kwenye kikaango cha kutoka kwamba, anatabia za kitoto

Friday, July 23, 2010

Kanye Wizoo aopoa mtoto wa kiKenya baada ya kumwagana na demu wake..!


Rapa Kanye West ameonekana kuhamishia penzi lake kwa mtoto mmoja mkali ambaye ni model huko UK huku akiwa amezaliwa Kenya.
Mtoto huyo anachukua nafasi ya model Amber Rose ambaye ndio alikuwa demu wa mnyamwezi Kanye huku akiwa anauhusiano na Shay.
Demu amechanga damu ya kiItaliano, Kenya, kireno na ki-arab.

This reports come after US Weekly magazine reported that Kanye broke up with Amber because he’s diving into his music. “Kanye is consumed with recording his comeback record in Hawaii and had to shut it all off. When he’s in work mode, he can’t handle a relationship. He told Amber he needs to devote everything right now to his craft.”

ASHANTI UNITED YAANDAA DUA YA KUMKUMBUKA MAREHEMU DITOPILE


KATIBU Mkuu wa klabu ya AShanti United ya jijini Dar es salaam Haji Bechina kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo wamepanga kuwaombea dua marehemu wote waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo itakayofanyika katika shule ya msingi Boma Ilala jijini Dar es salaam
Bechina aliwataja watakaosomewa duwa hiyo kuwa ni pamoja aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyekuwa Mlezi wao Rajabu Mgodo, Athumani Nobi waliokuwa makatibu katika vipindi tofauti na Mzee Mwalimu Kinyogori ambaye alikuwa mwenyekiti.

Bechina alisema kuwa klabu zote za mpira wa miguu zilizopo jijini DAr es salaam pamoja na wadau wa mchezo wa soka wamepewa mialiko kwa kushiliki dua hiyo itakayofanyika jumapili hii ya julai 25
Aidha klabu hiyo imepanga kuisuka upya timu ya soka ya AShanti United baada ya kupoteza mwelekeo miaka ya hivi karibuni.
Mbali na soka AShanti pia hujishughulisha na uinuaji wa vipaji vya mchezo wa ngumi kupitia kocha Rajabu Mhamila Super D
Bechina aliongeza kuwa wanajivunia timu hiyo ya ngumi ambako mchezaji wao Joseph Richard, alimpiga kwa KO ya raundi ya pili Kijepa Omari katika pambano la utangulizi kabla ya Rashidi Matumla na Mada Maugo kwenye ukumbi wa P.T.A, ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam

Monday, July 19, 2010

Ali Kiba aibiwa demu Mombasa, Kenya....!


A coast based promoter Sly Moses has denied allegations fronted by Tanzanian singer Ali Kiba, accusing him of stealing his girlfriend.


The two apparently had a falling out because of Hilda Manyala aka Hilly Baby who is said to be dating the Bongo flava heartthrob. Sly denied the allegation that he had stolen the singer’s girl adding that Ali Kiba was just out to create hype for his new single and no such incident occurred. Ali Kiba has since released a diss track aimed at ridiculing Sly for stealing his lover. The single Mtaka Cha Watu is enjoying airplay in Mombasa based FM stations.

Thursday, July 15, 2010

BIG BROTHER ALL STARS HOUSE tayari kwa mtanange mpya kuanzia July 18...!


M-Net today released sneak peek images of the new, refurbished Big Brother Africa house and the transformation from the tough, gritty Revolution to the sensational ALL STARS version is complete…with the photographs showcasing a contemporary, streamlined and luxurious atmosphere that encapsulates hi-tech means Hollywood glam!





Kaa tayari mdau kwa BIG BROTHER ALL STARS! Kumbuka series/mtanange huo utaanza saa 2 kama kawa (19.00 CAT) siku ya jumapili July 18 kupitia channel ya DStv namba 198 chini ya program za M-Net and AfricaMagic.


KTK SHOW ya ufunguzi; mtu mzima SEAN PAUL ol tha way from Jamaica anatarajiwa kusababisha.........!



Diamond amkaanga 'Tanzanite'.......!

Tanzanite aka Abdul Flava

CHAMA cha haki miliki Tanzania (COSOTA) kimezuia kupigwa kwa wimbo wa msanii chipukizi wa Bongo Fleva Mwingereza Athuman ‘Tanzanite’, ujulikanao kama ‘Kafara’, imefahamika.

Hatua hiyo inafuatia chipukizi mwingine wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ kupeleka mashitaka cosota akidai kuwa Tanzanite amenakili wimbo wake wa ‘Mbagala’. Tanzanite ambaye pia anajulikana kama Abuu Flava alisema kabla ya kurekodi wimbo huo aliongea na Diamond na kumuomba kufanya hivyo, alimkubalia lakini anashangaa baada ya kutoka akaenda kushitaki Cosota.

Alisema licha ya Diamond kuitwa katika vikao vya usuluhishi cosota alikuwa hatokei na mwishowe maamuzi yakatolewa, hata hivyo anasema amekubaliana na maamuzi hayo na hana kinyongo chochote.

Tanzanite alisema kilichofanya Diamond ageuke ni baada ya kuona ‘Kafara’ ni mzuri kuliko ‘Mbagala’ ndiyo maana ameingiwa na hofu, lakini hata hivyo amejipanga kikamilifu katika medani ya muziki na anatarajia kutoa nyimbo bomba zaidi.

Maamuzi ya COSOTA ni kama yafuatavyo.........

1. COSOTA watatoa matangazo kwa FM Radio zote kupiga marufuku wimbo wa KAFARA usichezwe tena!

2.Itabidi Abuu Flava amlipe fidia msanii Diamond kama akitaka.

Em, Drake watamba Top 200 Billboard wiki ya 3


Wasanii wa Hiphop Marekani Eminem na Drake aka Drizzy wamezidi kutamba ktk chati za Billboard Top 200 kwa wiki ya tatu sasa, huku ma-nigga wengi wakikataa kukubali ukweli kwamba Em anatisha ktk album yake ya sasa ukilinganganisha ya ile ambayo wengi waliifagilia zaidi ya Slim Shady......


Top 200 Album Sales (Top 5 Hip Hop/R&B)

Rank Artist Album This Week Est. Total

1 Eminem Recovery 229,000 1,287,000

2 Drake ThankMe Later 74,000 783,000

3 Big Boi Sir Lucious Left Foot:
The Son of Chico Dusty 62,000 63,000

12 The-Dream Love King 23,000 82,000

17 Usher Raymond v. Raymond 19,000 918,000

Monday, July 12, 2010

Waasi wa Somalia 'Al Shabaab' washukiwa kuua watu 64 wakiangalia Fainali ya Kombe la Dunia Uganda...!

mama akilia kwa uchungu karibu na mwili wa ndugu yake aliyefariki ktk shambulio hilo.


Watu 64 wamekufa papohapo na wengine kujeruhiwa wakati wakiangalia mechi ya fainali ya kombe la dunia kupitia Tv ktk mgahawa wa Ethiopia huko Kabalagala, karibu kabisa na Kampala. Vifo hivyo vilitokea baada ya wanaosadikiwa kuwa waasi wa kikundi cha al-Shabab cha Somalia kulipua mabomu wawili. Al - Shabab wanaonolewa na kupewa mafunzo na maaskari wastaafu kutokea Afghan, Pakistan, na Iraq wapo chini ya Al Qaeda, bomu lingine walilipua Kyadondo Rugby Club iliyopo Nakawa ambapo pia watu walikuwa waki-chek fainali hiyo kati ya Spain na Uholanzi usiku wa jana.


Inasemekana magaidi hao walikuwa wakiwalenga Wamarekani, waEthiopia na Uganda, serikali za Marekani (kupitia kwa waziri wake Bi. Hillary Clinton) na Uganda zimetoa pole kwa waathirika wote

“I join President Obama in strongly condemning today’s attacks in Kampala, Uganda targeting innocent spectators watching the World Cup final,” Clinton said. “We understand that American citizens may have been injured or killed and our embassy is reaching out to assist. Our condolences go out to the families and friends of the victims, in the United States and Uganda.”

sehemu moja ya umati wa wa-Tanzania wakifuatilia fainali hiyo jijini Dar es salaam

Friday, July 9, 2010

WAKAZI - NIPO POTE Lyrics

Wakazi, msanii from Tanzania livin in USA
Verse I
Nimeiteka dunia nzima/
Nahili swagga langu la kiutu uzima/
Full kujiachia mwanangu huwezi kupima/
Kama Dar kila jiji wakazi nina zizima/
Of course Chi huitaji maswali/
It’s the most special baada ya Ukonga stakishari/
Nina wana who hold me down mashariki ya mbali/
sehemu ambazo kwenda lazima uvuke bahari/
Kwanza twende Helsinki ndani ya finland/
Yupo binamu Goshashy na big dogg Bya/
Huko mimi nikitinga misosi Napata na Beer pia/
Na naendeleza utamaduni wa kitanzania/
Ulaya nzima mpaka alipo Beatus Wambali/
Whos the father of all knowledge pia ni MTU HODARI/
Uzalendo wenu daima huwa wa vitendo/
Ndo maana nawa salute kwa amani na upendo/
lets go!


chorus
Kila kona mimi nina mashabiki/
Magharibi kusini kaskazini na mashariki/
Ugh follow me kama maneno huyasadiki/
Im everywhere na hiyo ni sababu ya muziki/
Kila kona mimi nina mashabiki/
Magharibi kusini kaskazini na mashariki/
Ugh follow me kama maneno huyasadiki/
Im everywhere na hiyo ni sababu ya muziki/



Verse II
Nna mashibiki mpaka bara la asia/
Watu ambao nyimbo zangu nazo hawajawahi kusikia/
Ila kwa moyo wote bado wanashangia/
Ukiwauliza kwanini eti swagga linawavutia/
Ukienda UK yupo Fau so Real/
Im good on the daily ndani ya hivyo visiwa/
From Leicester, Manchester, Leeds to London/
Liverpool, Edinburgh, Wales, mpaka Birmingham/
Ya’ll got beautiful girls moyo wangu wanautibu/
Wananipa ninachotaka na tena bila aibu/
Shout out to Sanka, William Sereki, King Tibu/
Kenneth Mwazyunga Blackberry message hebu zijibu/
Mashabiki kila kona wasanii wananionea wivu/
Ndo maana kila nikikicha mimi wanaanzisha bifu/
Huwezi amini nna ma fans yaani mpaka ujerumani/
Kila kona ya dunia utadhani mbuni ramani/





chorus
Kila kona mimi nina mashabiki/
Magharibi kusini kaskazini na mashariki/
Ugh follow me kama maneno huyasadiki/
Im everywhere na hiyo ni sababu ya muziki/



Verse III
Ukirudi mtoni Iowa yupo Nsia na J Hux/
Kwa zake kick na snare its always a good look/
Michigan Grand Rapids n Detroit they make noise/
Shout out to Bfinest, Kawa na Chingaboy/
Hali yenu ya hewa inafanana na Chi/
Ndo maana kimuziki mimi ninaendana na Gwaii/
West coast sio siri mimi sijawahi fika/
Ila soon nitajiri Ms. Ouellette kanialika/
Pia kwa Edwin Mtei Konyagi mpaka tapika/
Total knockout, kwa T K nitapita/
Kisha nikitoka hapo ni straight dirty south/
Where all the girls at, LBT whats up/
From Texas to Atlanta na napo ni nyumbani/
Shoutout to Sajo, Justehll, Carlos na Karabani/
DC, Maryland, Virginia yupo AJ Ubao/
So utamaduni unaendelea kama mkuki na ngao/
Word up Faith, Young Replay and Dee Money/
Kay and Lillian see aint a damn thing funny/
Tennessee yupo Big Thabeet/
Massachusset Springfield yupo Lil Thabeet/
Without forgettin out the Big city of New York/
David Daz holds me down plus ma nigga Dru York/
Goerge na Stanboi hold me down in Kansas state/
All the way to Florida, I’m in state to state/



chorus
Kila kona mimi nina mashabiki/Magharibi kusini kaskazini na mashariki/Ugh follow me kama maneno huyasadiki/Im everywhere na hiyo ni sababu ya muziki/




Yeah shoutout to Columbus Ohio you know what Im sayin, you know I love ya’ll man…Ukonga, Chicago ya already know what it is…Albino Fulani, Jackie MissTanzania, Phat Black, Chibo, Kondwani, Akili Mtaalam, DJ Kvelli, Mkwawa Siblings, Sophia, Mohamed Mohamed, U know I remember…Indiana, Benny Sikare whats Up!! Wisconsin, Boston, Franklin Word up!Massachusett, Dee Sombe The Swagga Continues hahaha….Dallas, maaan Daudi, Abdillah Kinyaga u know what im sayin…Nigeria, Demola Fashola whats up man?!Tennessee Nashville, Yuzo word up? I love you my brother......

Zain kuipeleka Uganda MAMAs awards 2010...!


Makavu Blog imeinyaka news kwamba Zain MTV Africa Music Awards (MAMA) inatarajia kufanyikia Uganda. Zain wameamua kupeleka sherehe za awardz hizo Uganda Kulingana na mafanikio makubwa waliyoyapata huko, mpaka sasa waandazi wa event hiyo wapo wakitafuta kiwanja kizuri kitakachofaa kuibeba MAMAs awards 2010, na inawezekana wakafanyia Lugogo Cricket Stadium kwa kuwa ni kubwa na inaweza kuhimili pilika za MAMAs.

Thursday, July 8, 2010

Matumla, Maugo kuzichapa Julai 18 PTA Sabasaba....!

Mjasiriamali wa mpambano wa ngumi, Selemani Semunyu katikati akiwa na mabondia Rashidi Matumla (kushoto) na Mada Maugo wakati wa kutangaza mpambano wao wa kirafiki utakaofanyika julai 18

BONDIA mkongwe wa ngumi za kulipwa nchini, Rashid Matumla 'Snake Man', anatarajia kuzichapa na mpinzani wake Mada Maugo 'Junior', katika pambano lisilokuwa la ubingwa litakalofanyika Julai 18 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba Dar es Salaam.Akuzingumza na waandishi wa habari jana, Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania'TPBO', Yassin Abdalah 'Ustaadh' alisema kuwa mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni Julai 18 mwaka huu.

Alisema kuwa pambano hilo la uzito wa Middle lenye raundi 10, linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na historia za mabondia wote.Abdalah alisema kuwa wameamua kuandaa pambano hilo ili kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa ngumi nchini.

Alisema kuwa pambano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Media Entertainment & Sports Promotion na linaratibiwa na TPBO.

Ukubwa Dawa...!

Dj Ruge bosi wa primetime promo na radio Clouds akisugua mashine kuweka mambo sawa ktk onyesho la Fiesta Morogoro......

AY na MwanaFA wamsapoti 'Sista V' kugombea Ubunge Rukwa...!


Mwanamuziki wa kizazi kipya Abwene Yesaya akimkabidhi shilingi laki moja kwa Katibu msaidizi wa Idara ya Itikadi na Uwenezi pia ni Mjumbe wa NEC Chama cha Mapinduzi CCM, Violet Mzindakaya kwa ajili ya kwenda kuchukulia fomu ya kugombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa Rukwa pesa hizo zimetolewa na wasaniaa Hamisi Mwijuma 'mwana FA na Abwene Yesaya AY kwa ajili ya kumpa sapoti kijana mwenzao ili aende kuwawakilisha vema bungeniMSANII wa Muziki wa kizazi kipya nchini Ambwene Yesaya 'AY' na Hamisi Mwinjuma 'Mwana FA', kwa pamoja wamemchangia sh. 100,000 mjumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) Violet Mzindakaya 'Sister V' kwa ajili ya kuchukua fomu ya ugombea wa nafasi ya viti maalum Mkoa wa Rukwa.
Shime vijana wengine wenye uwezo jitokezeni kuwania nafasi za uongozi wa ktk uchaguzi mkuu ujao, tuko pamoja na tunawasapoti sana!!! - Makavu blog.

SHYROSE BHANJI Kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni...!


Shy-Rose Bhanji ajitosa ubunge jimbo la Kinondoni

· Asema mwaka 2010 ubunge unahitaji tafsiri mpya
· Aainisha maeneo nane atayoyafanyia kazi
· Kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana
· abainisha umuhimu wa ofisi kila kata ndani ya jimbo

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shy-Rose Sadruddin Bhanji ametangaza kujitosa katika nafasi ya ubunge jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia CCM na lengo lake kubwa ni kuwa kiungo muhimu katika jamii ya wanakinondoni.

Akitangaza azma yake ya kuomba ridhaa kwa wanachama wa CCM katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Shy-Rose alisema kwa mtazamo wake neno ubunge kwa mwaka 2010 linahitaji tafsiri mpya kabisa. `…kwa sasa mbunge anatakiwa kuwa ni kiungo cha jamii badala ya kuwa mwakilishi wa jimbo kama ilivyozoeleka` alifafanua Shy-Rose.

`Mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko na ndio maana nimeona kwamba ili kila mwananchi kuweza kuwajibika, nafasi ya mbunge inahitaji kutafsiriwa upya ili iendane na wakati na matatizo ambayo yanayotukakabili wananch` alisema.

Wa-Kenya wazindua Tuzo mpya Afrika Mashariki...!


Swahili Nation Music Awards (SWANMA) has been officially launched.
The awards motto Let's Go Global is a call for East African musicians to think beyond the continental borders.
Word has it that Talk Back Thames Television, the sponsors of X-Factor, have already expressed interest in supporting the awards, which are intended to become regional awards for the Swahili speaking nations.
The awards CEO Brian Kasoma said, SWANMA will be on promoting music done in English, which he looks at as a marketable language.

Ya Pweza yawa kweli...!

Utabiri wa Pweza aliyepewa jina la Paul wa Ujerumani "Octopus oracle" umewaumiza ma-fanz wengi wa Ujerumani ktk michuano ya Kombe la Dunia huku pweza huyo akiendelea kujiwekea rekodi za ukweli baada ya kutabiri kuwa Germans watapigwa na Spain usiku wa jana.

Tayari alishatabiri matukio ya mechi 6 za ujerumani, huku wengi wakimchukia pweza wao kiasi cha kutaka kumkaanga na kumfanya supu......

Tuesday, July 6, 2010

OMMY G; RUDI MWANA lyrics


Ommy G mwanaHiphop mwenye style ya pekee Bongo aliporudi tena ktk fani mwaka 2007 baada ya ngoma yao ya kwanza aliyoimba mwaka 2001.


OMMY G featuring DKNOB

Song: RUDI MWANA
Producer: Marco CHALI
Studio: KamaKawa Record, yr 2007


Intro;

(Dknob); Bwana Ommy G naona ndio unarudi
(Ommy G); Eeeehe!
(Dknob); Usitukane lakini
(Ommy G ); Situkani..!

Chorus; DKNOB

Kama mkali ndio mla nyama, hauhitaji kisu
Style yako mundu wenyewe watainama
Kama kurudi, rudi mwana hauhitaji ngenga
Only matendo yataongea sana.

Verse I;

I never thout before, kama ningeweza kuinuka na kusimama tena
Kwani wasionipenda walishanikatisha tama na kuwekeana dau
kwamba sitoweza kuinika na kusimama tena,
wengine wakajitokeza kunichukia,
they hate me, they hate my life, they hate me all
wakachukia mpaka the way that I was dressing
lakini wanangu wachache ndio mkanipa moyo
mkanambia mtu wetu kazaaa
haya maisha chukulia simple ipo siku utatoka
leo namshukuru Mungu tupo pamoja tena
tunakula ganja na kunywa, na mademu wa matawi yale yale yakina Langa
wana, wanangu, nilikaa chini sasa nimeinuka na nnaamini ipo siku ntatembea
na mtoto wa kihuni maisha yangu yatakuwa oya oya!
Chorus; DKNOB

Kama mkali ndio mla nyama, hauhitaji kisu
Style yako mundu wenyewe watainama
Kama kurudi, rudi mwana hauhitaji ngenga
Only matendo yataongea sana.

Verse II;

Kama kuja ndo mmeshakuja na ndo mmesha bugi,
Kwanza mmenikuta starter mixer ngada, tat for tat
Mtoto wa kihuni mmenikuta nipo na Dknob
Halafu ile makodinda makostamina
Yaani mmenikuta niko physical mashit makali
Nyie mmekuja kikauzu mie mmenikuta kimbubu
Mimi ni diamond nyinyi ni dhahabu
Gharama yangu ni kama ya D lakini mimi niko very expensive
Kihivyo habari ndo hiyo na haya ni Makavulive!
That is my lifestyle
Hii ni style yangu mimi na wanangu nipe changu
Umeyakanyaga umeyatimba umeyagalambua na lazima ligalambuke!
Chorus; DKNOB

Kama mkali ndio mla nyama, hauhitaji kisu
Style yako mundu wenyewe watainama
Kama kurudi, rudi mwana hauhitaji ngenga
Only matendo yataongea sana.
Nyimbo ipo namba 5 kwenye Playlist ya Makavulive hapo juu
Unaweza KUSIKILIZA na KU-DOWNLOAD Buree kabisa!

Ndio zetu.... huku kwetu ndo zetu..!

madingi tokea pande za nyanda za juu kusini wakigida ulabu kwa kutumia ndoo na kidumu bila ya kujali kitu... kwan huku ni kama kawa tu!


Ronaldo ashangilia kupata kitoto cha kiume....!


Mwanandinga machachari wa Ureno Cristiano Ronaldo (25) amefurahia sana kuwa baba baada ya mwanamke aliyemlipa pesa nyingi ili amzalie mtoto kujifungua kitoto cha kiume june 17, Ronaldo ameonyesha furaha yake jana kupitia Facebook na Twitter huku akitaka watu wasihoji na kutomtaja mwanamke aliyemzalia mtoto huyo wa kiume.



It is with great joy and emotion that I inform I have recently become father to a baby boy. As agreed with the baby’s mother, who prefers to have her identity kept confidential, my son will be under my exclusive guardianship.


No further information will be provided on this subject and I request everyone to fully respect my right to privacy (and that of the child) at least on issues as personal as these are.”

Monday, July 5, 2010

Kiongozi Muasisi wa Hezbollah afariki.....!


Muhammed Fadlallah died today from internal bleeding from liver disease. In case you don't know, he was the mastermind behind Hezbollah (the Party of Allah), arguably the most successful terrorist movement on earth. He was 75.

Hezbollah was the victor in the Lebanese Civil War that lasted through much of the 80s and 90s. There were about 17 armies (not kidding) fighting each other in this war.

The US Marines were driven out of Lebanon due to a Hezbollah truck bomb attacking their barracks and killing over 200 US Marines. UN rules prevented the Marines from shooting at the truck as it approached their base, allowing it to get through the gate and detonate. This led to a breakdown in US-UN relations, which has had severe effects on the world ever since (like the Iraq War, Somalia, etc).

Hezbollah has battled Israelis for decades and in 2006 drove them out of Southern Lebanon in armed combat, taking over 1000 casualties in the brief war (Israel lost about 100 men then ran away).

It will be interesting to see who takes over Hezbollah now and how it will affect the relative stability of the Middle East.

http://www.foxnews.c...test=latestnews


ZIFF kuanza julai 10 Zanzibar...!

Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF,Dr. Martin Mhando akifafanua jambo kwa wadau waliofika katika mkutano wa ufunguzi rasmi wa tamasha hilo katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar. Mkutano ulifanyika jumamosi julai 3.
Mratibu wa Maswala ya Muziki wa ZIFF,Edward Lusala (kushoto) akitaja list ya wasanii watakao panda jukwaani katika tamasha hilo linalotazamiwa kuanza rasmi Julai 10 mpaka Julai 18 huko kisiwani Zanzibar.wengine toka kulia ni Dean Nyalusi (Meneja wa ZIFF),Dr. Martin Mhando (Mkurugenzi wa ZIFF) na Ibrahim Mitawi (Msaidizi wa mambo ya Kiufundi ZIFF).
Baadhi ya wadau walifika katika ufunguzi rasmi wa tamasha la ZIFF katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar wakifuatilia kwa makini maelezo ya Dr. Mhando (hayupo pichani)..


ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL


Zanzibar International Film Festival (July 10th-18th) ni tamasha kubwa kuliko yote ya utamaduni ya aina yake kwenye ukanda wa Afrika mashariki. Ikiwa imetimiza miaka 13 na kuudhuriwa kila mwaka na zaidi ya wageni 200,000 na kushirikisha nchi 43, ZIFF ni taasisi ya wazanzibari yenye kulenga zaidi filamu za kiafrika huku ikisherehekea na kuthamini utajiri wa tamaduni zilizopo ndani ya ukanda huu na zaidi

Tofauti na tamasha lingine lolote, hili ni tajiriba ya aina yake ya tamaduni za kiafrika. Hakuna zuria jekundu, Umaridadi na waandishi wa habari za udaku.

ZIFF ni tamasha linalokuja mara mmoja tu kwa mwaka, ni nafasi ya pekee kwa Wazanzibari kujumuika pamoja na kutazama filamu kwenye viwambo vikubwa. Kwa mwaka huu filamu zote zitaonyeshwa bure kwa wakazi wote wa Zanzibar!


ZIFF’s theme this year’s is Hopes in Harmony.
Mwishoni mwa mwaka huu Zanzibar itafanya uchaguzi mkuu wa serikali. Kuna historia ya machafuko kipindi cha uchaguzi kwa kutazama uchaguzi uliopita mwaka 2005 kati ya wanaounga mkono upinzania na polisi. Mbiu ya tamasha kwa mwaka huu ina angaz matakwa ya watu wa kisiwa hiki ya amani na muafaka.

Filamu ya ufunguzi, ni filamu yenye tunzo inayo muhusu mwanamziki maarufu Youssou N’Dour, I Bring What I love (Naleta nachokipenda), inayozungumzia ]addresses the themes of religious tolerance, harmony and peace.

“I Bring What I Love” imedhaminiwa na SIGNIS.


Key Facts & Figures in 2009
• Waudhuriaji Mji Mkongwe: 45,000
• Waudhuriaji Dar es salaam: 200,000
• Wageni toka nje: 12,000
• Nchi zilizo shiriki: 43
• Filamu zitakazoonyeshwa mwaka huu: 100


Vitu Vya Kutazamia Mwaka Huu…
Fainali ya Kombe la dunia! Kwa kuzindua tamasha 2010 tutaonyesha mechi ya fainali ya kombe la dunia ndani ya Ngome Kongwe.

Filamu ya ufunguzi
Youssou N’Dour. I Bring What I Love Ni filamu yenye tunzo nyingi. Ya kuhamasisha, inayotupeleka kwenye safari ya kimziki, yenye ushuhuda wa nguvu ya sauti ya mtu mmoja kuhamasisha mamilioni. Muongozaji wa Filamu: Elizabeth Chai Vasarhelyi. Imedhaminiwa na SIGNIS.

Nipe Jibu: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza . Filamu ya kwanza ya kuchanganya Muziki na kuigiza Muongozaji Nadine Louise Fasera. Nipe Jibu ni filamu nzuri ya Kiswahili yenye kuchanganya muziki iliyotengenezwa kwa mtazamo wa kisasa na kitamaduni kwa simulizi iliyochangamka juu ya binti yatima anayeishi kwenye maisha ya ndoto.

My Policy: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza. Kijana mdogo mfanya biashara anapigwa risasi kwenye siku yake ya kuzaliwa akiwa anarejea nyumbani kwake akitokea kwenye tafrija yake kusherehekea siku hii muhimu akiwa na mchumba wake, Victoria. Wiki chache baadae, Yule aliyempiga risasi amjia na kumchoma kisu hadi kufa. Kwa kupagawa na pigo hili, Victoria aamua kuhama Montreal na kuanza maisha mapya, Lakini muuaji amjia nay eye pia.... Muongozaji: Phad Mutumba

Motherland: African premiere - Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Africa

Ana’s Playground: African premiere

Lamu’s Maulid: world premiere

Inside Life: world premiere
Pumzi: East Africa’s first ever science fiction film
A sneak preview of Twiga Stars

Muziki
ZIFF 2010 Itakua ikisakata kwenye burudani ya muziki na… Dully Sykes – AKA Mr Misifa ama Mr Chicks, Msanii anayetambulika sana kwa miondoko ya dancehall Tanzania. AY, Msanii anayengara ndani ya Africa Mashariki akiwakilisha vyema Tanznia na balozi wa burudani Tanzania, Kidumu , Ndiye mwanamuziki maarufu Africa Mashariki toka Burundi anayeshikilia Tunzo nyingi ikiwemo tunzo ya Muziki bora wa Afrika Mashariki kwa Tunzo za Tanzania Music Awards, Body Mind Soul Bendi ya watu 6 kutoka Kaskazini mwa Malawi wanaopiga mziki wa kiafrika wenye vionjo vya Jazz, Windhund featuring Sekembuke & Siga bendi kutoka Austria inayotumia vionjo vya kizungu na kiafrika, ushairi na sanaa ya simulizi ili kuleto vionjo vipya na vya aina yake kwenye ulimwengu wa muziki.

Filamu za Watoto!
Kwa kushirikiana na taasisi ya filamu ya Kidanish, Maonyesho ya filamu za Watoto zitaonyeshwa makundi makubwa ya Watoto, zikiwa zimetafsiriwa kwa Kiswahili kwajili ya Watoto na vijana wa Mji mkongwe.

Art exhibtions
"Hopes in Harmony" (Matumaini yenye Kuafikiana) – Onyesho la picha yanayoletwa na mpiga picha toka Italy, Carlo Deste
"Colour Bash" – Uchoraji wa vitenge kutoka pande mbalimbali za Afrika, na Mahelia de Randamie
Artwork kutoka wakina mama wa Iranian, Hii inaletwa na Ubalozi wa Iranian embassy
kwa kushirikiana na Soko Filam, ambapo watengeneza filamu na wachongaji toka Zanzibar wanakuja kuonyesha na kuuza bidhaa zao..

Tasnia
ZIFF ni tukio muimu kwenye jumuiya ya Cinema duniani. Festival Forum na Festival of Festival program inatoa nafasi kwa wasambazaji, mapromota, waongozaji wa filamu na waandaji kukutana ili kukomaza mizizi kwenye tasnia ya filamu kwenye nchi zinazoendelea. Mwaka huu wawakilishi toka Trinidad na Tobago, Uganda, Holland, Iran, Mexico and Italy watashiriki ZIFF kujadili nafasi ya matamasha ya filamu kwenye nchi zinazoendelea.

Warsha
ZIFF itaendesha warsha tatu wakitoa upendeleo kwa ushiriki wa waandaji filamu toka ukanda huu wa Afrika mashariki kwa waandaji wenye kuonyesha hari na vipaji vyenye mlengo wa kuibuka kwenye tasnia hii.

WARSHA ZA NAMNA YA KUOMBA MISAADA YA KIFEDHA KUANDAA FILAMU NA WARSHA – warsha itaongozwa na wakufunzi toka Sweden and Uganda

UANDAAJI WA MAKALA: CONNIE FIELD – Warsha hii ya siku nzima italeta mtazamo mzima wa namna ya kuandaa makala chini ya usimamizi wa mshikiliaji wa tunzo ya uandaaji wa makala(producer / director), Connie Field.

CINEPHILMS:UTENGENEZAJI WA FILAMU KUTUMIA SIMU YA MKONONI – Hii warsha ya aina yake itaongozwa na Jonathan Dockney wa chuo kikuu cha Natal South Africa. Utengenezaji wa filamu kwa kutumia simu za mkononi ni teknolojia inayo ibuka kwa kasi sana. Njo ujifunze jinsi ya kutengeneza filamu kwa simu!

Tafadhali bonyeza hapO kwa maelezo zaidi:
www.ziff.or.tz
ama
www.ziff.or.tz/press

Asmah Makua
(Swahili Press)
asmahmakau@yahoo.co.in
Tel no: 0713711413
Laura Martin-Robinson
(English language Press)
press@ziff.or.tz
Tel: +255 782689845

Saturday, July 3, 2010

TWO in ONE' ol flava under one roof....


Miss Kinondoni 2010 apatikana..!


Miss Kinondoni 2010 Alice Lushiku akiwa katika picha ya pamoja na warembo wenzake baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Miss Konondoni lililomalizika Dar es salaam jana kwenye ukumbi wa Mlimani City, kulia ni mshindi wa pili Amisu Malick na mshindi wa tatu ni Irene Hezron na wa nne Edna Kwisasa na tano Carolene Mbembo

Miss Kinondoni 2010 Alice Lushiku akiwa katika picha ya pamoja na warembo wenzake baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Miss Konondoni lililomalizika Dar es salaam jana kwenye ukumbi wa Mlimani City, kulia ni mshindi wa pili Amisu Malick na mshindi wa tatu ni Irene Hezron na wa nne Edna Kwisasa na tano Carolene Mbembo
Alice Lushiku akijibu swali
Irene Helron akijibu swali
Edna Kwisasa akijibu swali

Caroline Mbembo akijibu swali wakiti wa onesho hilo ata hivyo alichemka kujibu baada ya kutaja mbuga ya Serengeti ni Mlima mkubwa alichemka vibayaa sanaaa

5 bora


mrembo mwenye kipaji cha kucheza akicheza



Carolene Mbembo mrembo mwenye kipaji cha kuimba

ISSA MNALI AKIWA KAZINI


kamati ya miss Ilala wakiwa na warembo wa Ilala wakiwasoma wenzao


wadau wa urembo na habari walikuwepo Selemani Mbuguni 'papaa' na Khadija khalili


wanenguaji wa bendi ya twanga pepeta wakiwajibika jukwaani

Suzan Chubwa Queen Suzi akifanya vitu vyake wakati wa kumtafuta Miss Kinondoni