Tuesday, May 29, 2012

MISS DAR INTERCOLLEGE KUJULIKANA JUNI 8, SUN CIRRO

SHINDANO la kumsaka Miss Dar Intercollege 2012 linatarajiwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Sunciro, ulipo Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam, imefahamika.
Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba warembo watakaoshiriki shindano hilo wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na Bob Rich.
Alisema mpaka sasa warembo 12 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamesharipoti kambini.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga, Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus,Jane Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.Taji la kitongoji hicho linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.
Kwa upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.
“Tunaomba makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano letu…mpaka sasa wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na Clouds Fm.

CMpoo aachia track 2, "Who iz Next" na "Voicemail"

CMpoo,hiphop Mc mwenye makazi yake pande za Ungalimi chugatown,anakuja na pini mbili mpya,"round hii Mc's nawapa Hiphop & Ragga Joint nilzopiga pande za noizmekah.com,track ya voicemail ni mkono wa Moscow na mixing kasmamia Defxtro,na pini la "who ni next" ni ragga riddim nimerecord noiz juu ya beat la kijamaica,Mbali na music napiga artwork mtaa,Graffitti na signwork katika business area mbalimbali kama maduka na mabango,music ni passion yangu japo hailipi bado ila mipango yangu ya hivi karibuni ni kuigiza filamu,Big up kwa fans wangu na wadau wote katika game la hiphop!!!!...

Monday, May 28, 2012

KIMBUNGA KUWARUDISHA KWAO WASANII WALIOKUJA DAR KUTOKEA MIKOANI

Kimbunga, pic from Swahilioriginol

Chini TONGWE REC. mnyamwezi amefanya dude jingine kali safari hii akidhamiria kwa makusudi kabisa kuwarudisha makwao wale wakali wa HiPhOp Bongo,

Mchizi anasema ye yupo DownTOWN kitambo......
Sasa anamrudisha kwao yule alitoka Dom (sijui nani labda Cowboy)
Af anasema anamrudisha fid Mwanza kisha mzidi maarifa
Kisha anamrudisha wa Tanga halafu na yule wa Arusha huu mwaka wa 10 toka aje mjini hajarudi kwao kijijini, alimpokea mwenyewe na kibegi cha MonTaNa.... ENDELEA KUMSKIZA MWENYEWE KTK PLAYLIST HAPO JUU!!!

Kawashirikisha ROMA, DOMOKAYA, na JOS MTAMBO
 

DJ - TASS LIVE NDANI YA TRIPPLE A, ARUSHA 1st JUNE

Arushaaaaaaa,sasa Stopa Rhymes,Izzo Bizness,Ommy Dimpoz Veejay, May C na wasanii wengine kibaooooooo!!!!
watakuwa kwa stage siku ya Ijumaa terehe moja mwezi wa sita mwaka 2012 

Pande za Arachuga ndani ya Ukumbi wa The Triple A Blue Fame,
performance za kueleweka ndani ya usiku huo unaoletwa kwenu na Talet survivor a.k.a Deejay Tass toka Pro 24 Deejays!

Come one come all..

MAKAMUZI YA DIAMOND EVICTION SHOW YA BBA.... IK AMFANANISHA NA R. KELLY

 Diamond kama kawaida yake alikamua vilivyo ktk Eviction Party ya BBA StarGame jana usiku kiasi cha kushangiliwa sana na baadhi ya fans walijaribu kupanda stejini ili wacheze nae lakini wakazuiliwa na Baunsa

 Mampi kushoto akiwa na shosti wake Maneta kabla IK (picha ndogo) ajampa taarifa za kutolewa ndani ya jumba la BBA 

Thursday, May 24, 2012

Fido atoka na HipHop-JamaicAN "HustLinG"

Fido,Kiongozi wa vatoloco the Red anadhihirisha uwezo wake katika Chantin pon dem riddim beats kama jinsi mzee wa style tatu; stoppa rhymez hufanya,kwa namna alivyotembea ki-hiphop juu ya beat ya toka jamaica "Watu wananifahamu zaidi kwa hiphop tracks zangu na support niliyo nayo kwa ragga artists hapa home,and this tym im lettin the world know arachuga is tha kingston of tanzania,we gat the best w**d out here man! ask anybody!Fido anadrop pini hili la "Hustling" ambalo lipo katika upcoming mixtape yake ya "VatoRiddims" volume one...enjoy it rasta!

Hapa Kazi tu, Udashosti pembeni!

Vijana Kazini! Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba, akikaribishwa makao makuu ya Vodacom Tanzania na Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa wateja wakubwa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba. Naibu Waziri huyo alifanya ziara hiyo ya Utambulisho Vodacom na kukutana na uongozi mkubwa wa kampuni hiyo!

Pini Jipya kutoka kwa Middle Rymez "DEGREE"

Middle Rhymes toka chugatown ni Upcoming HardcoreHiphop M'cs wenye mood na hii game,ikiwa ni pini lilosukiwa beat na mzee mzima mosco na vocal pande za noizmekah.com, middle rhymes wameonyesha uwezo mkubwa sana ndani ya hili pini,Enjoy

Wakazi - Excalibur

Tuesday, May 22, 2012

WIZI WA KAZI ZA SANAA KUFIKIA KIKOMO!

Mtendaji kutoka Kampuni ya Global StandardOne (GS1), Andrew Karumuna akionesha moja ya kazi ya Msanii Judith Wambura(Lady Jay Dee) iliyowekewa alama maalum ya kimataifa ya utambuzi na udhibiti wabidhaa kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.Lady Jay Dee ni msanii pekee ambayeamekwishaingia na kuanza kunufaika na mfumo huu.

 
 Bi. Fatma Kange akiongea na wadau wa Sanaakuhusu mfumo maalum wa kimataifa wa utambuzi na udhibiti wa bidhaa mbalimbaliwakati akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari, BASATA GodfreyLebejo na Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego. 


Na Aristide Kwizela, BASATA
Huenda kilio cha wasaniijuu ya wizi wa kazi zao kikapungua kama si kufikia kikomo iwapo wasaniiwataamka na kushirikiana na kampuni ya Global Standard One (GS1) ambayo imekujana mfumo wa kimataifa wa kutambua na kudhibiti kazi za Sanaa.

Akizungumza wiki hii kwenyeJukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo Fatma Kange alisema kuwa, mfumo huo wa kuziwekea alama ya utambuzi yakimataifa (barcode) kazi za wasanii utasaidia kudhibiti uharamia kwenye sektaya sanaa na kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi.

“Mfumo huu ni wa kimataifa,umekuwa ukitumika duniani kote miaka 38 iliyopita, hapa kwetu ni mpya kabisa.Ni mfumo wa kutambua bidhaa halali kwa kuziwekea alama maalum (barcode) ambayoitazifanya zitambuliwe kimataifa na kutokughushiwa” alisema Bi. Kange.

Friday, May 18, 2012

CANDY aachana na 'Most Records', sasa anapiga mzigo na NASS B 'PAMOJA RECORDS"

STUDIO YA "PAMOJA RECORD" IMEACHIA SINGLE MPYA YA YULE MWANADADA CANDY AMBAYE MWEZI MMOJA ULIOPITA ALIACHIA NGOMA YAKE INAYOKWENDA KWA JINA  NIMPENDE MILELE IKIWA CHINI YA MOST RECORD..!.
LEO HII "PAMOJA RECORD" IMEACHIA SINGLE YA MWANADADA HUYO INAYOKWENDA KWA JINA LA "CHANINI", CANDY MSANII AMBAYE LICHA YA UIMBAJI PIA ANAKIPAJI PIA CHA KUCHEZA MIZIKI  YA AINA ZOTE.
 

CANDY AMBAYE MTAANI ANAJULIKANA KWA JINA LA (CANDY TIKISA!! AU CANDY WA KUJIACHIA..!) , AMBAYE AMEJIPATIA UMAARUFU MKUBWA PALE ALIPOSHIRIKI MASHINBDANO YA KUCHEZA MUZIKI  YALIYOKUWA YANAJULIKANA KAMA "TIKISA" AMEACHANA NA LEBO YA "MOST RECORD " NA KUPATA OFA NYINGINE KWENYE STUDIO ZA PAMOJA RECORD JIJINI DAR ES SALAAM, AMBAYO TAYARI AMESHAREKODI SINGLE YAKE HIYO MOJA INAYOITWA "CHANINI" AMBAYO TAYARI IMESHAANZA KUPIGWA KWENYE VITUO MBALIMBALI VYA REDIO. KWANINI AMEACHANA NA MOST RECORD?................. CANDY ANAJIBU  KUWA HAWAKUELEWANA NA MANAGEMENT NZIMA YA MOST RECORD AMBAPO KWA SASA WAPO KWENYE MZOZO AMBAO BADO HAUJAPATIWA UFUMBUZI  LAKINI TAYARI ALIKUWA AMEREKODI SINGLE MOJA  PAMOJA NA VIDEO AMBAYO VYOTE AMEFANYIA KWENYE KAMPUNI HIYO YA MOST RECORD,  YEYE CANDY AMEIZUIA ISIONYESHWE KWENYE VITUO VYA TELEVISION MPAKA PALE MUAFAKA WAO UTAKAPOMALIZWA.

CANDY AMEWAFAGILIA SANA PAMOJA RECORD KUWA WAPO SAWA NA MAKINI SANA KWENYE KAZI NA NDIYO MAANA AMEINGIA MKATABA NAO NA HUKO ATAFANYA KAZI AMBAYO MASHABIKI WA MUZIKI WATASUUZIKA NA MUZIKI WAKE.................EBU SIKILIZA SINGLE YAKE HII YA CHANINI............ NDANI YA WIMBO HUU AMEZUNGUMZIA KITU GANI!! ...........EBU FUTATILIA ALA ZA MUZIKI JINSI GANI ZILIVYOPANGWA NA KUPANGIKA CHINI YA USIMAMIZI WA MKUBWA  WA MTAYARISHAJI WA MUZIKI  MTU MZIMA NASS B.

Wednesday, May 16, 2012

Baada ya Kutemana na 'La Familia', 'CHIKU K' atoka na Sharks Family "UTAISOMA"


Kundi la Sharks Family ni mkusanyiko wa wasanii ambao wameamua kuunda
umoja wao na kujiita sharks Family ambao ndio wamechokoma na Single
yao ya kwanza... 
Humo ndani utabahatika kusikia sauti kama ya Man
Setta, K Sal (Mzee wa Mkiwa), Chiku K na wengine wengi.

Artist: Sharks Family
Song: Utaisoma
Prodyucer: Steve White

Wanahitaji Saport kabisa kwani wamejitahidi.

BOU NAKO - JEMBE LA KASKAZINI


Mzee mzima D Double anayejulikana vema zaidi kama BouNako a.k.a Jembe la kaskazini anadondosha dudeee brand new kwa fans wote wa hiphop duniani..hii ndio "Jembe la kaskazini"(download hapa),ikiwa ni single inayofata "Mara Hoo" ambayo imefanya vema mtaa na media kwa miez mitatu ilopita, "Game ni gumu tangu enzi za baba zetu likini kukata tamaa sio suluhu wala haisaidii, nakomaa kwa maana mashabiki zangu ndio wananipa nguvu ya kutifua" hii ni zawadi kwenu kwa support yenu kununua T-shirt za J.E.M.B.E na iko wazi mimi sio kitu bila ninyi, skilizieni more tingz zinakuja "walete" pamoja na "acheni"..

Tuesday, May 15, 2012

Wakazi - Heartbreaker

Duh, Obama 'mchicha mwiba'

Rais Obama aki-kiss na David  Cameroon

Obama aki-kiss na Chavez
It won't be nearly as controversial as Time magazine's breastfeeding cover, but Newsweek's May 21 issue declares Barack Obama the country's "first gay president."
The accompanying cover story was written by Andrew Sullivan, the popular--and openly gay--political blogger. The magazine even gives the commander-in-chief a rainbow halo.


Obama, Sullivan writes, "had to discover his black identity and then reconcile it with his white family, just as gays discover their homosexual identity and then have to reconcile it with their heterosexual family."
The full cover story is not yet online, but in a blog post published earlier this week, Sullivan wrote that Obama's support of gay marriage brought him to tears:

Sunday, May 13, 2012

Happy Mother's DaY!!

Afeni Shakur alipata ujaozito wa Tupac akiwa Jela,

Tupac aliwahi kufungwa Jela, akiwa jela alitunga huu wimbo kama TRIBUTE kwa Mama yake!!

HAPPY MOTHER'S DAY

Wednesday, May 9, 2012

MISS NYAMAGANA KULINDIMA JUNE 2, GOLD CRET MWANZA






Shindano la Miss Nyamagana 2012/2013, linatarajiwa kufanyika usiku wa Jumamosi ya terehe 02 June 2012 katika ukumbi wa Gold Crest Jijini Mwanza. Takriban warembo 25 wamejitokeza katika shindano hilo, huku idadi ya warembo kujaza form za ushiriki ikiongezeka kila kukicha.

Mazoezi kwa warembo yataanza rasmi tarehe 14 June 2012 katika ukumbi wa Gold Crest Mwanza. Kwa mawasiliano ya udhamini na ushiriki kwa warembo piga namba 0717 557 220, 0764 088 48.

A-CITY BOYZ waachia 'More Than", Baada ya kutoka Ghana...!


Contagious B-Boys a.k.a A-CITY BOYS; Kundi la dancers mahiri from ChugaTown ambao pia wanaimba music,wanadrop brand new ragga dancehall track ijulikanayo kama "More Than" na hii ni kazi ya kwanza tangu turudi kutoka Ghana kwenye mashindano ya kudance! humu ndani katika hii track amezungumziwa manzi mkali anaesumbua jiji na tumerocord audio hii kwa defxtro apa apa chugatown"

 Contagious wenye maskani yao pande za arachuga wamekua bize zaidi wakijifua mashairi na sauti kwaajili ya kumudu music game vilivvyo,Waburudishaji hawa pia wameahidi kung'ara zaidi katika medani ya kuvunja majoka a.k.a.Breakdancing kwa vile team yao sasa imeongezeka dancers wapya na vile vile mazoezi yanakwenda kiubunifu zaidi,


Shukrani milioni nane ziende kwa mafans wetu na wadau wote katika media ndani na nje ya bongo pamoja na dunia nzima!!!

SKIZA TRACK ZOTE MPYA KTK PLAYLIST YA MAKAVU

New Sound; EffectZERO "Com n Gerrit"

Wanadada EffectZero wanakwambia we gwan rock the scene this year coz we the best,we have faith in our management;Batoo Ent & the JamDropa deejays,our producers and most of all our fans" na hivi ndivyo inavyokuwa maana sasa wanadrop brand new joint yao kama crew,Pini linakwenda kwa jina "Com n Gerrit" yaani njoo upate,Mamdundo kama kawaida pande za noizmekah.com kwa Defxtro na this tym around tunafikiria kurecord couple more jointz hapa na pale tukiendelea kujipanga ku-launch our singles in selected clubs roun town!!!!Much love to all tha radio deejayz who bump our track,more coming yo way sooner than u think! EZ Baby!!

New Sound; HUYU SHORY - B Man ft. MirryCandle & Slimdizzy


Bman, yule yule wa "Bonge la toto" enzi  ya "HOTPOT" family awashirikisha Kc toka  FBG,mdada MirryCandle pamoja na Slimdizzy toka Northdwellers,

Wote wakiwa ni artists toka kaskazini mwa tanzania pande za arachuga,collabo hii ya kipekee sana kwani ni ya kwanza iloweza kuwakutanisha baadhi yao kwa mara ya kwanza,Idea ya hii track niliipata tu nikiwa mishemishe za kuuza tshirt zangu mpya za "MY STYLE" kwa mtaa,

 Nikamchek Defxtro ambaye alinipa mwongozo zaidi katika kuisuka kuwa collabo unique zaidi na pia kuipa ladha ya dancehall vile,Otherwise hii naitoa straight from noizmekah.com kwa fans wangu wote Tanzani ana Duniani Kote,Nawapenda sana kwasababu mnaniamini...

JEMBE JIPYA KUTATUA MASLAHI YA WASANII BONGO

Mh. Fenela Mukangara


Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dk. Fenela Mukangara akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya IKULU jijini Dar es salaam, hivi karibuni

Alipoishia Dk. Nchimbi ni pazuri sana kuendelezea na kufikia safari yetu ya KUDAI MASLAHI YA WASANII NCHINI TANZANIA!!!
Our eyez On U Mheshimiwa.

KIINGEREZA KINAWAKWAMISHA WASANII WA BONGOFLEVA KIMATAIFA...!

Mpaka kuwa judge wa TPF5 auditions ni recommendation ya HERMY B wa B-Hitz kwa project manager wa TPF5..Ikiwa ni mara yangu ya pili kuwa judge wa music contest,mara ya kwanza ikiwa ni katika "Serengeti Fiesta Freestyle" ya arusha zone ilofanyika "mawingu club arusha,nikisaidiana na judge mwenzangu,hiphop Legendary FidQ" akapatikana mshindi "Tash Tashnificent wa chapia" na second runner up "VeeJay wa Kimziki Zaidi",

Nimejifunza kwamba Tanzania tunaweza sana muziki,changamoto kubwa inayotukabili ni tabaka la idadi ya wasanii wanaozungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

Kenya wana idadi ndogo ya Music Artists likini wenye mafanikio na mikataba mikubwa na makampuni tofauti na Tanzania wasanii wetu ni wengi sana na wengi wao hawana mikataba wala endoresments za kufanya wajiendeleze kimaisha,


Tofauti inakuja kuwa Kenyan artists wapo wachache na wote wanamaintain status kwa miaka nenda rudi because ufanisi wao wa mawasiliano kwa kiingereza kunageuka "ticket" ya kufanya ziara nyingi zaidi nje ya nyumbani kuliko ndani hivyo kubaki RELEVANT over TIME

Thursday, May 3, 2012

Baghdad "Pray G Kweka" ni mwanafamilia wa Freemason!?



Pray god kweka jina la stage.
 Baghdad ni msanii alieeanza muziki ki mazabe sana na kuonekana kupata bahati ya kupewa saport ya ghafla mara baada ya kupewa nafasi ya kuonyesha kipaji chake mwishoni mwa tamashaa la kutoa nafasi kwa vijana wanaochipukia kwenye mziki wa hip to hip hop ambalo lilizuriwa na wasanii wakubwa wa ndani na nje ya nchi kama fid q, langa, Saigon, na wasanii waliotoka nje ya nchi ni gnl zamba, na msanii kutoka nchini nijeria ambae jina lake halikuweza kupatikana na miongoni mwa waandishi habari walioweza kuwepo kwenye tamasha hilo ni pamoja na fatma hasan, a.k.a fetty, ruben ndege a.k.a ncha kali ambae ni production manager wa clouds fm. 


Na kati ya maproducer wakongwe walionekana kuvutiwa na kipaji chake ni producer mkongwe Ali baucha ambae aliweza kutoa ma mc wengi wakubwaa wa hip hop Tanzania kama Fid q, Rado, Chid benz, na wengine wengi. Ndipo kukutanishwa na Manyeko na kufanya ngoma yake ya kwanza iliyoitwa “hip hop imesimaama” na kuweza kumfanya kuweza kujizolea mashabiki kibao kwa kuwa aliiachia siku moja baada ya kutolewa kwenye shindano la freestyl mc shujaa, ya mwaka 2009  iliyokuwa inaendeshwa na fetty chini ya kipindi cha bongo flava. 


 Na ukuaji wa mziki wake umekuwa wa ajabu ajabu kutokana kuwa mc wa kwanza Tanzania kufanikiwa kuwa na mashabiki wengi, kupiga shows nyingi kubwa, kufanya intaviews nyingi, kupewa promo na radio zote Tanzania bila kumbania ingawa mpaka alipofikia hana na hajawahi kuwa na manager wa aina yoyote na kila sehemu huwa anafanikiwa kufanya kazi bure na kujikuta wale wanaomfanyia kazi ndio kugaramika. 

Mfano baucha aliondoka na ngoma 5 na hakudaiwa hata shilingi 100 licha ya kutokuwa na makubaliano yoyote ya kusighn na studio ya baucha! 
Amefanya ngoma mbili ambazo zimefanya vizuri sana ndani na nje ya nchi full ng’ae ng’ae bila kutoa hata sh 50 kwa producer wa d fatality na hata baadae walipokuja kukorofishana aliweza kuja kufanya ngoma ya ohh mama na climax bibo, na wakati hawakuwa wakiongea na producer aliefanya mix bila malipo, wakati messen alikiri ya kuwa ufanyaji kazi wake umebadilkika kwa sasa pesa mbele kama tai.


 Na kwa sasa anakabiliwa na kesi kubwa ya kutumia chater ya kundi alilokuwa akilitumikia mwanzoni mwa mwaka 2010 kabla ya kujitoa mwanzoni mwaka huu, na chaa ajabu uliwahi kusikia wapi mtu aliyepeleka kesi mahakamani kama mdai alietambulika kwa jina lililopo kwenye file la kesi DiCkison kuomba suluu baada ya kuhairishwa kesi mpaka tar 3 mwezi May.

 Hivyo hali yake ya kuwa anaogopewa na watu wengi kila sector, Inaweza kudhihirisha ya kuwa yeye ni muhusika wa familia ya freemason, kwa kuwa hajawahi kufanya show hata moja asiwe kati ya wasanii watatu bora kwenye show hiyo, na lazima ataonyesha vidole, au ishara yoyote ya ajabu. Baghdad, a.k.a Notorious wa bongo, kwa sasa anatumia jina la P.G Kweka au Mjukuu wa Lusifer.

 

Kuhusiana na mziki

 Video ya “hip hop imesimama” kunapicha ya fuvu, ukicheki "kamba 2kamba" kuna ishara za free mason, ukpitia baadhi ya lyn zake, mfano kwenye hip hop imesimama
     “ marehemu ninaeish kiufupi mi nmzmu
     Tanzania nw brnda  dar n bidhaa hadimu
      sijasomea majungu na wala siujui umbea
     doubt nilipo sasa usiulize nilipotokea”

     kwenyengoma yake ya “ng’aeng’ae” alisema “nawauzunisha waliojipaga kuelekea moton nawa furaisha wenye tv yakuona pepon

 kwenye ooh mama  “yee ni zombie joo mzimu wa marehem huwa hauzirai” 

kwenye kamba 2 kamba aliziirisha dhahili kuwa anatoa kafara kwa kunywa damu zawatu kwa kusema “damu za dadazao zinatolewa kafara ghetto” licha ya ngoma mpya  ambayo ukisikiliza lyn moja baada ya moja  kumuusisha na freemason kwa kukiri kuwa yeye ni Mjukuu wa Lucifer, jina la kiongozi wa free mason! 

Na moja ya line zake anasema ‘was bon freemason na ubongo alipewa na lusifer, been haso kutafuta damu awe satisfy.

 Na ukiisikiliza mwishoni mwa ngoma hii utasikia akisema dissline kwa "Diamond platinum" na huwezi amini kwa msanii mkubwa kama Diamond ambae ukionekana kugusa hata kiatu chako kwa soli yako haoni shida kukufungulia kesi ila imekuwaje kuwa kimya kwa kauli hii kutokuifanyia kazi!

BouNako na Majembe pande za Empire Sports Bar

BouNako,MoPlus,Lady Fire,BadTaito,Yung Omega,Wachaina,DopBoy na Mc's kibao watakua pande za empire sports bar inside Shoprite complex tarehe 4 May 2012 kupiga show heavy ya hiphop na ragga kwa hisani ya Empire,93.0 MJ fm Station Arusha na Noizmekah Studios

show hii itakua hot,kwa kiingilio cha elfu tano TU!

Libeneke la CHUMA

Natumai nyote ni wazima wa afya,nashukulu sana kwa kuzidi kunipokea wadau wote na wale wanaoona umuimu wangu.

Nawaletea libeneke Kwenu. Blog  mpya ya CHUMA BLOG ambayo  itakuwa ikikuletea Habari ,Burudani, Michezo, Maisha na Jamii inayo kuzunguka . Karibuni sana ukiona Link hii mpatie na mwengine. 

Natanguliza Shukrani zangu kwenu Asanteni Sana.

Kutembelea Libeneke hili Bofya hapa:  

CHUMA HABARI
:  
www.salimchuma.blogspot.com
 
pia kwa sasa kutakuwa na link ya
   
 CHUMA BURUDANI:  www.bongoflavalink.blogspot.com

Dr. Dre kushiriki filamu ya 'Thaw'



MUIGIZAJI na nyota wa singo ya 'Kush the man himself' rafiki wa karibu na Tupac  yuko mbioni kuanza  kufanya filamu iliyopewa jina la “Thaw”.

Filamu  itaandikwa na  Vick Weet, Kutoka Variety habari zinasema Andre Romelle Young ama Dkt. Dre ataifanya filamu hiyo na rafiki yake Daniel Schnider ambae ndo ameleta wazo hilo.

Filamu itahusisha mashetani ambayo yatakua yanatokea kwenye barafu, Dr. Dre sio mgeni Hollywood, Dkt. Dre.  ni mwanzilishi na mmiliki wa sasa Aftermath Entertainment na mmiliki mshiriki wa msanii wa zamani
wa studio ya Death Row Records, na pia mtayarisha albamu kadhaa kwa ajili yake na wasanii wengine kadhaa wa rekodi hiyo kama vile Snoop Dogg na Eminem.

J . COLE kupagawisha On the Openning of BIGBROTHER STARGAME!


 Rappa na Producer J.COLE aka Jermaine Lamar Cole ( January 28, 1985) anatarajiwa kupiga ngoma zake kali 3 ktk Bonge moja la SHOW ktk ufunguzi wa Bigbrother Africa Code 7, (BigBrother StarGame) siku ya jumapili May 6 ambapo washiri zaidi ya 30 wanatarajiwa kuingia ktk Jumba la BBA na kuanza mtanange huo ambao utaishia siku ya 91 kwa mshindi mmoja kuzawadiwa zaidi ya Tshs. Milioni 400.

We are giving Big Brother Africa fans across the continent, the once-in-a-lifetime opportunity to have hip hop megastar J.Cole answer a burning question they’ve been dying to have him answer!

Since the news broke out that talented Roc Nation signee J. Cole will be performing at the StarGame Live Launch on Sunday, May 6, the Social Media buzz has been deafening.

And why not since the man is not only serious eye candy, but has a Grammy nod backing his already stellar credentials. Now, Big Brother is giving you the opportunity to put the man in the hot seat!

It’s simple really. All you have to do is connect with us on Facebook or on Twitter and post questions that could be used in our exclusive web interview with the American superstar, which will happen 15 minutes before the start of the Live Launch Show.

Wednesday, May 2, 2012

Jessica apiga picha za Utupu!


MWANAMUZIKI  Jessica Simpson ameamua kufuata nyao za wasanii wenzake
maharufu,mara baada ya kupiga picha za utupu akiwa na ujauzito wake wa
pili.


Mpaka sasa wasanii ambao wameshapiga picha za utupu wakiwa na ujauzito
ni Britney Spears,Christina Aguilera,Mariah Carey,Demi Moore,Claudia
Schiffer ,Cindy Crawford,na wengine wengi Mwaka huu mwanamama Jessica
Simpson Ametokea kwenye Jarida la ELLE Magazine..

Bondia Fike aachana na masubwi kwa mapenzi ya mkewe!!

BONDIA na mtunisha misuli maarufu Fike Wilson mwishoni mwa wiki iliyopita amefunguka na kudai mke wake anamchanganya katika mapenzi ndio maana alisikiliza maneno ya mama mkwe na kuamua kuweka kando kazi yake.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Wilson alisema kuwa aliacha  mchezo huo aliodai ni wa kifo  mara baada ya kuumia katika mpambano wa mwishoni kabla ya kustaafu masuala hayo baada ya kuwa ameumia bila kupigwa konde lolote ulingoni.

"Kabla ya kuamua mie mwenyewe kuacha kupanda ulingoni , mama mkwe wangu ndio aliye sema niache ndondi kwani siku hiyo ya mpambano wangu mwaka 2005 nilijikwaruza wakati wa mchezo wangu huo nikaumia ulingoni jeraha lilikuwa kubwa lilimsikitisha mama mkwe,"alisema Fike.

Tuesday, May 1, 2012

Linex aachia bonge ya Ngoma...!!

MSANII LINEX WENGI WANAPENDA KUMWITA  "MJEDA" AMEACHIA NGOMA YAKE MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA "AIFORA', IKIWA NI SINGLE YAKE YA 3 KUACHIA MWAKA HUU TANGU UANZE, NGOMA YAKE YA KWANZA KUACHIA ILIKUWA "MACHO YANGU JUU"  BAADA YA HII AMEACHIA SINGLE NYINGINE INAITWA "NITAIFICHA WAPI" SINGLE AMBAYO AMEMSHIRIKISHA MSANII DIAMOND AMBAYO INAFANYA VIZURI SASAHIVI KWENYE VITUO MBALIMBALI VYA REDIO, LINEX AMEACHIA MZINGO MWINGINE MATATA SANA.....
HAKIKA WIMBO HUU UKIHUSIKIA UTAKUKUNA SANA....
WIMBO AMBAO UTAKUJA KUFANYA VIZURI SANA WIMBO HUU MPYA AMBAO UNAITWA "AIFORA" UMESIMAMIWA NA PRODUCER ANAYEITWA  "FUNDI SAMWELI". HAYA KAZI KWENU WASIKILIZAJI NA MASHABIKI WA "MJEDA LINEX" NA MKAE MKAO WA KUSUBIRI VIDEO YAKE YA WIMBO HUU AIFORA..!


WIMBO :- AIFORA
MTAYARISHAJI WA MUZIKI :- FUNDI SAMWELI
MSANII : LINEX

Miss UKONGA 2012 Patachimbika Mei 5!!


Warembo wa Ukonga wakiwa katika picha ya pamoja.Mashindano ya kumtafuta Miss Ukonga 2012 kitongoji cha jijini Dar es Salaam, yanendelea kwa kasi katika Ukumbi maarufu Hill tec uliopo Ukonga, Banana, jijini Dar es Salaam ambapo warembo hao wanadai kila moja atakuwa mshindi katika shindano hilo.

Mazoezi hayo yalishuhudiwa na Miss Tanzania wa sasa, Salha Israel, na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga. ambao walitoa ushauri kadhaa kwa warembo hao.
Fainali ya mazoezi hayo itafanyika Mei 5 mwaka huu katika Ukumbi wa Wenge Guarden ulipo Ukonga